Nandagala One
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 1,913
- 2,286
Wakuu Salam.
Bob Junior Simba Mtawala wa Serengeti hifadhi ya Serengeti ambaye ambaye alitawala kwa miaongo isiyopingua mitatu.
Bob junior alivuma kwa utawala wa kibabe ndani ya hifadhi yeye na vijana wa familia yake.
Alipendelea utawala wa kiimla, na Kujiona Serengeti ni yeye na yeye Serengeti katika muktadha wa utawala wa wanyama.
Hakupenda mashauriano na simba wenzake, kitu kilichosababisha simba wenzake kuanza kujipanga kwa lengo la kumuondoa madarakani himaya ya Serengeti.
Mpaka bob junior anakufa kifo katili, na Simba vijana aliowalea na kuwa gloom mwenyewe , alishuhudia majaribio kama 10 au 9 ya kumuondoa.
Jaribio la mwisho lilifaulu kwa kumlarua vibaya,akiachwa na majeraha ya kutisha mwili mzima.
Simulizi la Bob Junior Simba halina tofauti na sakata la Umwenyekiti CHADEMA Freeman Mbowe na uongozi wake ndani ya CHADEMA.
Anguko la Bob Junior ni la kisiasa katika himaya ya wanyama, na anguko linalotarajiwa la Mbowe kutoka madarakani ni la kisiasa pia katika muktadha wa siasa za binadamu, kwa taasisi ya CHADEMA.
Mbowe anataka kutolewa madarakani baada ya kukwepa majaribio mengi.
1.Jaribio la Chacha Zakayo Wangwe.
2.Jaribio la ZITO Kabwe na kitila Mkumbo.
3. Nia thabiti ya Tundu Lissu, Heche na kanda mbalimbali ambazo zinampinga kama Bob Junior alivyokuwa anapingwa hifadhini na Simba wenzake.
Nionavyo kama Bob Junior alivyoanguka kisiasa na kupata MAUTI MWILINI ,ndivyo Mbowe anavyokwenda Kuanguka KISIASA TU BILA MAUTI YA MWILI.
Kama Mbowe anafikiri na kutafakari sawa, kwa heshima yake, kwa CHADEMA na Watanzania,akae pembeni kwa heshima, vinginevyo atakutana na sakata kama la Simba Bob Junior.
Mimi ni mwanafasihi , nimeamua kutumia simulizi la kweli la Bob Junior kumkumbusha Freeman Mbowe kuwa zama zake na wakati huu ni sawasawa na Zama alizopitia Bob Junior.
Tchao.
Nandagala One,kwa Sasa "CHAKO NI CHAKO DODOMA"