Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mbowe ni mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo amedumu madarakani kwa muda mrefu akijaribu kumfukuzia Baba wa Taifa kwa muda ambao aliiongoza TANU hatimaye CCM tangu uhuru hadi alipoamua kung'atuka kwa hiyari yake.
Ingawa tuampiga mishale mingi bwana Mbowe lakini ameendelea kuwa nguzo ya CHADEMA hasa kuelekea kwenye mitaguso ya kisiasa. Pamoja na kufanyiwa hila za kihuni na CCM kuitumia NHC kuporomosha biashara zake ambazo amezirithi kutoka kwa baba yake.
Hivi karibuni alikabiliwa na kesi ya kubumba ya ugaidi ambapo kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani, sisi kama jamii tulifunguka macho kugundua UKATILI mkubwa unaofanywa na CCM kupitia jeshi la polisi ambao wanatumika kudhibiti upinzani wa kisiasa dhidi ya CCM
Swali ambalo kama jamii ya wadadisi wa siasa za Tanzania tunapaswa kupata majibu ni kuhusu succession plan, kwamba baada ya yeye ameandaliwa nani kupokea kijiti kuweza kuipeleka CHADEMA kwenye kufanikisha malengo yake ya kuongoza dola kwa manufaa ya Watanzania?
Kiongozi makini ni yule ambaye anaongoza huku akiandaa watu wanaoweza kuongoza dira na malengo ya taasisi.
Uzi huu siyo sehemu ya shinikizo la kumtaka ang'oke madarakani