hakika kuna tatizo. Wakati wanachana wengine wa CHADEMA na hata Gazeti la Tanzania Daima wakithibitisha kuwa Ben alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, GODLITSEN Malisa, Kada maarufu wa CHADEMA ambaye naye alisemekana amepotea sambamba na Ben anaibuka na kusema tuipuuze taarifa ya Kuwa Ben alikuwa mkurugenzi wa Sera na Utafiti na kwamba taarifa hiyo ni ya uongo. Malisa anataka kutuambia nini? Kuna tatizo hapo. Mwanachama mwingine wa CHADEMA maarufu katika mtandao wa kijamii wa facebook, Kwinyara Kwintara Kwinyara anaandika shutuma nzito kwenye ukurusa wake wa facebook akiutuhumu uongozi wa CHADEMA kwa jinsi usivyochukulia kwa uzito suala la Ben, halafu kutaka kuonesha kuwa ataeleweka vibaya kwa viongozi wake anarudi anasema akaunti yake imeingiliwa. Hapo napo kuna tatizo. Malisa na Kwinyara Kwintara Kwinyara wote ni watu wako karibu sana MBOWE. Ukiunganisha haya ya Malisa na Kwinya na hii mada hakika, nadiriki kusema kuna giza totoro. Tumuombe tu Mungu aepushe haya tunayoyawaza. Tunaweza kutofautiana kiitikadi lakini linapokuja suala la uhai wa binadamu lazima muungane katika sintofahamu ya kila aina, sote ni wana wa adam.