Akiwa kwenye kampeni siku ya leo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema CHADEMA haitosusia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu kama ilivyosusa mwaka 2019 na kusema pamoja na changamoto za kuenguliwa kwa Wagombea wao bado wataendelea kushiriki Uchaguzi huo.
'Tuliwasusia mwaka 2019, kosa hilo haturudii tena safari hii tutabanana mpaka tone la mwisho la damu, hata wakiiba na wakifanya chochote tutatoka na mitaa ya kutosha na vijiji vya kutosha, asante Ndugu zangu wa Mbeya”