LGE2024 Freeman Mbowe: Tuliwasusia mwaka 2019, kosa hilo haturudii tena. Safari hii tutabanana mpaka tone la mwisho la damu

LGE2024 Freeman Mbowe: Tuliwasusia mwaka 2019, kosa hilo haturudii tena. Safari hii tutabanana mpaka tone la mwisho la damu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Akiwa kwenye kampeni siku ya leo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema CHADEMA haitosusia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu kama ilivyosusa mwaka 2019 na kusema pamoja na changamoto za kuenguliwa kwa Wagombea wao bado wataendelea kushiriki Uchaguzi huo.


'Tuliwasusia mwaka 2019, kosa hilo haturudii tena safari hii tutabanana mpaka tone la mwisho la damu, hata wakiiba na wakifanya chochote tutatoka na mitaa ya kutosha na vijiji vya kutosha, asante Ndugu zangu wa Mbeya”

Soma pia: Mbeya: Katibu Mwenezi CHADEMA wa Kata ya Iganjo akiwaombe kura wagombea


==========================================================

Inaonekana CHADEMA washajua namna ya ku-deal na CCM. Hakuna kususa mpaka kielewe!

 
Back
Top Bottom