Freeman Mbowe tumia msiba huu wa mzee Ally kuinvoke Peoples power ili kumpata Deusdedit Soka wakiwa hai kabla haijawa too late

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kwako Ndugu Freeman Mbowe.

Uwezo wa kusaidia kukomesha vitendo vya utekaji na mauaji nchini unao ila hujaamua "kukasirika" vya kutosha

Ndugu Mbowe, wewe ni mwenyekiti wa chama ambao makada wake wamekuwa wakitekwa na kuumizwa, haitoshi tu kukasirishwa na kuumizwa, bali inapasws ufanye jambo na jambo lenyewe ni kuinvoke peoples power ili watanzania wakiongozwa na nyie wanachadema mnaotekwa waende mabarabarani kulaani chinjachinja hii iliyoanza kuota mizizi nchini. Mdugu Mbowe ukijifanya wise sana utaendelea kuonekana fala na muoga mbele ya hawa madhalimu.

Usiiamini kirahisirahisi kauli ya Samia juu ya uchunguzi. Najua wewe na Samia ni maswahiba japo "kikazi", lakini hili la sasa nchini limefikia hatua mbaya, Waongoze wanachadema wakatae udhalimu huu juu yao kwa kuwaongoza kuingia mabarabarani kuonyesha hasira yao. Achana na hoja muflisi eti Watanzania waoga, kama Watanzania waoga basi nyie wanachadema ambao msingi wa chama chenu ni PEOPLES POWER waonyesheni watanzania wengine kuwa nyie siyo waoga na mnasimamia falsafa ya chama chenu.

Mheshimiwa Mbowe, CCM na serikali yake wanakuona "mzee wa hekima", kwamba utatumika tu kuwa kama mlinzi wa getini kupoza hasira za wanachadema, Sasa ni muda muafaka wa kusimama kama Mwneyekiti na kumtaka kila Mwanachadema kulinda uhai wa chama. Mauaji haya yanalenga kutia hofu zaidi wananchi, yanalenga kuwagopesha makada wako. Sasa chukulia hali hii kama EXISTENTIAL THREAT KWA CHAMA CHENU. Itisha wanachama wako na wananchi kamanda wahit the roads. HII NDO NJIA PEKEE YA KUKOMESHA UDHALIMU HUU

Ndugu Mbowe, Saa 72 ni critical katika upatikananji wa Deusdedit Soka iwapo utaitumia nafasi hii awareness na hasira ya umma juu ya mauaji ya Mzee Ally. Tumia Fursa hii kukumbusha umma kuwa siyo mzee Ally peke yake aliyetekwa. Waambie serikali na wananchi kuwa hauna imani na na usalama wa Deusdedit huko Aliko. Tumia nafasi hii kumdai Deusdedit Soka na wenzie. Ukipoteza fursa hii, joto la kifo cha mzee Ally likapoa, Deus na wenzie hawataapatikana. MBOWE SEMA JAMBO, FANYA JAMBO, WEKA PRESHA

Ndugu MBOWE, Uwezo wa kuwaingiza watu kitaa kwa mujibu wa sheria unao, Sababu za kuwaingiza watu kitaa unazo. NIA YAKO SASA TUNATAKA KUIONA NA ACTION TUNATAKA KUIONA MUOKOE SOKA NA WENZIE KWA MASS ACTION BARABARANI. TUMIA FURSA HII YA MSIBA WA MZEE ALLY KUFANYA HIVYO.
 
Shida yake mbowe ni kukosa ile power ya mobilization,Sasa akiishia tuh kusema kunja ngumi kunja ngumiii itasaidia Nini.
Mbowe, Zitto na wenzake sijawahi amini kama ni wapinzani 100% naamini wana % za umamluki hao naamini wakipewa mpunga tu wanawauza wananchi, afadhali Lissu, maalimu Seif rip, bab Duni hawa wana misimamo kidogo ila sio Mbowe
 
Shida yake mbowe ni kukosa ile power ya mobilization,Sasa akiishia tuh kusema kunja ngumi kunja ngumiii itasaidia Nini.

Hilo ni tatizo lake kubwa sana.
Naamini anajua fika kuwa akiwahtiaji wananchama 10000 wa CHADEMA tu walio committed kuingia kitaa kulaani mauaji na utekwaji wa mwananchadema mwenzao uwezo huo anao ila NIA YA HIVYO HANA. Anataka kufanya siasa za kihekimahekima!
 
Shida yake mbowe ni kukosa ile power ya mobilization,Sasa akiishia tuh kusema kunja ngumi kunja ngumiii itasaidia Nini.

Hilo ni tatizo lake kubwa sana.
Naamini anajua fika kuwa akiwahtiaji wananchama 10000 wa CHADEMA tu walio committed kuingia kitaa kulaani mauaji na utekwaji wa mwananchadema mwenzao uwezo huo anao ila NIA YA HIVYO HANA. Anataka kufanya siasa za kihekimahekima!
 
Watanzania wengi wako BIZE na Simba/Yanga Kubeti na Miziki. mpaka yamkute yeye ndio LABDA ataingia Barabarani LAKINI HAKUNA GERENTII.


Na hata mtu wake akiuwawa yeye atakuwa anafikiria urithi ulioachwa na mtu huyo kwamba azikwe ili process za MIRATHI zianze.

Hakuna KAZI NGUMU DUNIANI KAMA KUMKOMBOA MTANZANIA.
 
D.soka it already too late, waambie tu watu wawe tayari for bad news
 
Naunga mkono hoja, huu ukondoo utatumaliza
 
Mbowe is a business man. And as every good merchant does, is weighing the entirety of his actions and words on a scale of profit. If it doesn't yield profit then Mbowe throws it under the rug.

Expecting Mbowe to mobilize the masses is akin to chasing the wind.​
 
Mbowe has wasted a unique chance today by reacting angrily to people who were jeering and chanting "Resign" to the minister of home affairs when addressing the mourners.

It could have acted like a stepping stone towards disciplining the government if would have been left to continue.
 

Hilo ndo tatizo la Mbowe, anajifanya kuwa na busara kuliko busara zenyewe.

Tunahitaji constructive anger, siyi mtu kutumika kama Nyapara kuzima hasira za umma
 
As a merchant he weighed the odds, and saw no profit. Maybe he was afraid of reprisals from the State, especially against his businesses. His businesses have been his long time Achilles heel.

But I totally agree with you, this is a wasted opportunity. He could have exploited mourners' anger and channel their indignation of against Mr Massauni just to send a good message to the Government.

Although what we're discussing here is totally immoral against the dead, but I could have worked magic.

Minister of Interior booted out of a funeral by angry mourners. Quite a spectacle, I can imagine 🤣🤣​
 
Nipo pale hili litapita kama mengine yanavyopita kamwe mbowe hawezi kufanya hicho kitu siku chadema akipata mwenyekiti mpya hapo ndo utaona sasa mabadiliko halisi
 

Yaani kwa jinsi walivyomuondoa Mzee wa watu .... Chance ya hao vijana kuwa hai ni ndogo sana. Unless, Maza afanye interference kwenye hili asap.
 
Yaani kwa jinsi walivyomuondoa Mzee wa watu .... Chance ya hao vijana kuwa hai ni ndogo sana. Unless, Maza afanye interference kwenye hili asap.
They are confused now, hawajui waachie sasa kama wapo hai, au waendelee kukaa nao.

Kitendo cha kuwaachia sasa kitaonesha straight wao ndio watekaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…