LGE2024 Freeman Mbowe: Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo:

1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta.
2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.
3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti.

Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM.

Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote.

Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika.

Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu:

"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.

Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
 
Lissu alikuwa anahamasisha chadema "wachukue hatua kama watakavyoona" Cha qjabu yeye hachukui hatua hizo, anajaza ujinga watoto wa wenzake wanaumizana
 
Hicho ndiyo chama chenye sera, na kilichojipanga kinafanya ujinga huu?
Haya mambo yalipangwa muda mrefu tu
 
Lissu alikuwa anahamasisha chadema "wachukue hatua kama watakavyoona" Cha qjabu yeye hachukui hatua hizo, anajaza ujinga watoto wa wenzake wanaumizana
Haikuppi sifa ya ziada yoyote unapo amua mwenyewe kuwa mpumbavu.
Hii furaha unayo ipata kwa mTanzania mwenzako kuondolewa uhai wake itakuongezea nini maishani mwako!
 
Chama Cha Mashetani CCM hakuna cha maana wanachopanga kwaajili ya manufaa ya Watanzania. Mipango yao yote imejaa ushenzi mtupu.

Hawa watu ni mashetani!! Hivi mtu mwenye Roho wa Mungu, kabisa anaweza kumtoa uhai binadamu mwenzake kwaajili ya ucjaguzi?? Hakika haiwezekani. Ndiyo maana, kwa uhakika, tunasema hiki chama kwa sasa ni cha kishetani.

Mwalimu Nyerere huko uliko, wakati wa uongozi wako, ulihangaika sana kwa dhamira ya kuwaletea maendeleo na kuwapa unafuu wananchi wa Tanzania. Leo, chama ulichokianzisha kwaajili ya kuwasaidia watanzania, wenzio wamekigeuza na kukifanya kuwa cha kishetani, na kazi kubwa ya hiki chama kwa sasa ni kuwatesa na kuwaua Watanzania.

Tunaomba sana mbele za Mungu wetu, Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, aliyemfedhehesha farao na magari yake, na farasi wake; ukuu wake uifikie CCM na kuiingamiza, pamoja na mashetani yote yaliyomo humo. Wauaji hawa wa CCM, wabebe laana wao wenyewe na vizazi vyao vyote. Madaraka wanayoyapora, yasiwape faraja wala furaha yoyote bali mateso ya kujufia, yakateseke kuliko wananchi maskini.
 
"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.
Kwamba hata huyo askari polisi aliyeua raia mwema aliyekuwa anazuia kura bandia kuingizwa kituo cha kupiga kura, na yeye hawezi kushtakiwa?!!

Kama ndivyo, basi nchi imerejea utumwani rasmi, kwenye ukoloni
 
Kama taifa tuna safari ndefu sana za kuiondoa CCM. Hili lichama limekuwa zimwi ambalo linapora chaguzi waziwazi kabisa. Kilichofanyika uchaguzi wa serikali za mitaa ni uharamia wa kiwango kikubwa. Naamini zikijumlishwa kura zote zilizopigwa mwaka huu tutakuwa na wapiga kura zaidi ya mil 60. Maana kila kituo zaidi ya kura 150 au 200 zimeongezwa.
Inasikitisha sana!!!
 
Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo:

1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta.
2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.
3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti.

Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM.

Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote.

Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika.

Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu:

"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.

Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
Hivi ni kweli kama taifa, we've no way forward to act against all these brutalities? Kila mtu Sasa ni mlalamishi na mtoa habari tu. Let's be creative and innovate best way to make the hooligans accountable.
 
Back
Top Bottom