Freeman, Tundu, Salumu (FTS). Nani kaitengeneza hii "Three R" ya Tanzania?

Freeman, Tundu, Salumu (FTS). Nani kaitengeneza hii "Three R" ya Tanzania?

moshdar

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
2,421
Reaction score
1,234
Wakuu miaka ya nyuma kidogo kunako Timu ya Taifa ya Brazil Almaarufu wapiga samba kulitengenezwa kilichokuja kuwa moja ya kombinesheni hatari, makini na kali kuwahi kutokea katika ulimwengu wa kabumbu a.k.a gozi a.k.a. soka ambapo kombinesheni hiyo ilikuja kujulikana kama Three R, au 3R au ara Tatu ikimjumuisha mtaalam mwenyewe Ronaldinho, Rivaldo na Ronaldo (3R). Pass za hawa jamaa zikatokea kuwa mwiba na sababu ya vilio na huzuni kwa timu pinzani, ilikuwa ni hekaheka 3R wawapo uwanjani kulitandaza kabumbu...walipress, walichomekea, walichengesha na walitambaiza na kusambaiza...naam ilikuwa ni samba, samba la Brazili.

Sasa upo mfanano umejitokeza kwenye siasa za Tanzania ambapo ule muunganiko wa 3R ya Brazili kubumbuni unaonekana dhahiri kwenye Siasa za Tanzania ambapo kuna hii combination ya 3Commanders ya Freeman, Tundu na Salumu almaaruf FTS. Hawa jamaa hawakabiki, hawazuiliki, wanauchezeachezea mpira wanavotaka, wana chenga za maudhi, wanapiga matobo, visigino, wanagonga wan two wan two za kutosha yan. Majuzi Tundu (T) kakabwa kwa kuwekewe beki mamluki hatari lakin kuona hivo 3kamandas wamebadili mbinu ya mchezo na sasa mpira kapasiwa Salumu (S) mshambuliaji mwenye kasi na viwango, anayetembea juu ya mpira huku akichagizwa vyema na maestro wao Freeman (F) na sasa ngoma ni mtenge mtenge huko kunako dimbani.

Hii combination inacheza total football, wakishambulia wanapanda wote, wakishambuliwa wanashuka wote kudifendi....matokeo yake Timu pinzani ulimi nje, Timu pinzani wanacheza rafu, wana ofusaidi, wana hendibol, kiungo chao kimekatika na beki imepotezana...naam 3kamandas a.k.a FTS ni combination hatari sana...hili ni samba, samba la kibongo ndani ya siasa...kwa sasa mtanange unachezwa zaid kusini mwa uwanja ambapo F akishambulia kutoka kaskazini huko machame, T yupo katikati ya dimba pale kariakoo akiunganisha pasi za moja kwa moja kutoka machame anazielekeza kusini mwa uwanja kwake S. S anaituliza pale uwanja wa Nachingwea, anajikunja kama chatu, anaangalia kushoto na kulia na ajikunjua shuti kali mtambaaa wa panya, anaupeleka mule mule anamotagia kware na ni goooooooooool....watu oyooooo watu wewee

Dah! dah! dah.......eeeeeehe! eeeeehe! hawa FTS ni hatari hawa, ni combination matata, wanacheza a trained football na wakati huo huo huku kwa pembeni kuna mchagizo wa zitto na mtaalam mwenyewe wa Sawasawaaa a.k.a maalim Seif...hatoki mtu, hatumwi mtoto sokoni.

Watanzania sasa kazi mliyobaki nayo ni moja tu moja tu sasa...nayo ni kuwashangilia 3kamandas a.k.a FTS kwa kuhakikisha mawakala wote wanaapishwa kwa mujibu wa sheria 17 za mtanange huu, kwa kuhakikisha siku ya kupiga kura kila mtu anampigia kura T pamoja wapambe wake mbunge na diwani wa timu ya CDM na washiriki wao wa upinzani, kwa kuhakikisha baada ya kupiga kura mnakaa mita 100 kusubiri matokeo na kuhakikisha wakala wamepewa fomu za matokeo kwa mujibu wa sheria 17 za mtanange...na mwisho kabisa kuhakikisha mshindi halali ndiyo anatangazwa na asipotangazwa mshindi halali wote mnavamia uwanja na kumzulia kizaazaa refa wa mchezo huu......

naam mtoto na asitumwe dukani, ni mashuti ya mwana nikome mwanzo mwisho....ni kombinesheni ya 3kamandas a.k.a. FTS...ni samba....naam!!! Samba la Kibongo
 
Back
Top Bottom