Freemasons katika siasa na dini

5. Ktk biblia ni wapi imeandikwa kuwa Mnyama wa kwanza wa Ufunuo anayepewa Nguvu na kiti cha enzi na yule Joka ni Rumi? Maana tujuavyo sasa hatuna utawala wa rumi unaotawala dunia.
Katika Danieli 7 wametajwa “wanyama wanne” ambao wanawakilisha falme nne. Kumbuka mmyama wa 4 aliyetajwa katika Danieli 7 ndiye mnyama aliyetajwa katika kitabu chote cha Ufunuo. Hivyo hapa tutaangalia sifa za mnyama wa nne wa kitabu cha Danieli, na mnyama wa kitabu cha Ufunuo, kisha tutaangalia ni wapi hapa duniani ambapo sifa za mnyama zinatimizwa kikamilifu.

1. Mnyama atakuwa na uwezo wa kisiasa na kidini (kanisa na serikali).

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, AMEKETI JUU YA MNYAMA mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Mwanamke au bibi-arusi katika unabii huwakilisha kanisa.

Ufunuo 21:2 “…Yerusalemu mpya…umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”

Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.”

Mnyama huwakilisha taifa au ufalme

2. Mnyama atakuwa na kanisa & serikali vimekaa juu ya milima 7.

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana…mwenye VICHWA SABA na pembe kumi.”

Vichwa saba katika unabii vinawakilisha milima saba.

Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.”

Je hapa duniani kuna kanisa na serikali vimekaa juu ya milima saba?

“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic Encyclopedia, p 529.

“Je vilima saba vya Roma ni nini?

Roma inajulikana kuwa imejengwa juu ya vilima saba. Roma ilisemwa imepatikana wakati Romulus na Remus, wana mapacha wa Mars, walifika katika futi ya kilima Palatine na wakauanzisha mji, Vilima sita vingine ni Capitoline (kiti cha serikali), Quirinal, Viminal, Esquiline, Caelian, na Aventine.” –Geography.about.com

Kwa hiyo unabii huu wa Ufunuo 17:3, unaonyesha wazi kuwa mwanamke aliyeketi juu ya mnyama, amekaa juu ya vilima saba vya mji wa Roma. Kwa vyovyote, ni Vaticani na kanisa la Romani Katoliki ambavyo vimekaa juu ya milima saba, na kutimiza unabii huu. Danieli 7:23 inasema mnyama wa mwisho (Roma) anatofautiana na wanyama wengine watatu waliopita. Kwa hakika hakuna taifa wala ufalme mwingine ambao una kanisa na serikali, harafu kwa wakati huo huo umekaa juu ya milima saba. Ila ni kanisa la Romani Katoliki pekee.

3. Mnyama atatoka baharini

Ufunuo 13:1 “Kisha nikaona mnyama AKITOKA KATIKA BAHARI, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Bahari katika unabii huwakilisha watu/jamaa, mataifa, lugha.

Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.”

Ukatoliki wa Romani ulitokea ulaya ya magharibi pamoja na makutano ya “watu/jamaa, mataifa, na lugha.” Na kwa wakati huu kanisa la Romani Katoliki lina idadi kubwa ya “watu, mataifa, na lugha,” kuliko kanisa jingine lolote duniani mwote. Na sasa, baada ya kuanzishwa kanisa moja duniani, Juni 26, 2000, Papa alichaguliwa kama kiongozi wa makanisa yote ambayo yameungana na lake. Hii ilifanya kanisa liongezeke mara mbili. Na hivi karibuni, makanisa yote pamoja na yasiyo ya Kikristo yatatangaza kwamba Papa ni kiongozi wao mwema.

Na Juni, 2008 mataifa 174 katika mataifa 192 duniani, yana serikali zao zikiwakilisha Vatican. Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabii huu kwa ukamilifu.

4. Mnyama atatawala miaka 1260. (kabla hajapata jeraha la mauti).

Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataadhimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake KWA WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI.”

Ufunuo 12:6 “Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko mda wa SIKU ELFU NA MIA MBILI NA SITINI.”

Danieli 7:25 inaonyesha muda ambao angetawala mnyama, kama wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. Ufunuo 13:5 inauonyesha mda huu wa utawala wa mnyama, kama miezi 42, miezi 42 = miaka 3 na 1/2. Hivyo, ukiangalia kwa makini hapa utaona kuwa, wakati = mwaka 1, na nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka.

Kwa hiyo, wakati nyakati mbili nusu wakati = miaka 3 na nusu ya Danieli 7:25, au miezi 42 ya Ufunuo 13:5, au siku 1260. Mahesabu haya yanathibitishwa katika Ufunuo 12:6 ambapo inasema, “Yule mwanamke (kanisa) akakimbilia nyikani…wamlishe huko mda wa siku 1260.” Kwa hiyo miaka 3 na 1/2 = miezi 42 au siku 1260 ambazo mnyama angetawala kabla hajapata jeraha la mauti.

Bado, wengine watakataa na kusema, hapana, miezi 42 haiwezi kuwa sawa na siku 1260, kwa sababu miezi mingine haina siku 30. Lakini katika unabii mwezi 1 = siku 30. Mwanzo 7:11 inasema, mvua za garika zilianza siku ya 17 ya mwezi wa pili, na Mwanzo 8:3, 4. inasema kuwa maji yakapunguka mwishoni mwa siku 150, harafu safina ikatua siku ya 17 ya mwezi wa saba. Hizo ni miezi 5 tangu mvua zilipoanza. Kama ukigawanya siku 150, kwa miezi 5, utapata siku 30 kwa kila mwezi. Hivyo, miezi 42 ikizidishwa kwa 30 jibu litakuwa 1260. Kwa hiyo wakati, nyakati mbili, na nusu wakati, ni sawa na miaka 3 na nusu, au miezi 42, au siku 1260. Kwa hakika, Ufunuo 12:6 inathibitisha mahesabu haya inaposema kuwa watoto wa Mungu watakimbilia nyikani kwa muda wa siku 1260 wakati wa utawala wa mnyama (upapa).

Katika unabii siku 1 ni sawa na mwaka 1,

Ezekieli 4:6 “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.”

Kwanza kabisa tunatakiwa kujua ni lini kanisa la Romani Katoliki lilipata nguvu zote za kutawala kama “mwanamke juu ya mnyama” (kanisa na serikali), na kutawala kisiasa na kidini kwa wakati mmoja kama Ufunuo 17:3 inavyosema.

“Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327

Hiistoria inathibitisha kuwa upapa umeanza utawala wake kama “kanisa na serikali” mwaka 538 B.K. juu ya amri ya mfalme Jastinian, na chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius. Na unabii unasema mnyama (upapa) atatawala miaka 1260 kabla haujapata jeraha la mauti.


NAOMBA NIISHIE HAPA
 
6. Freemason, illuminat vimetajwa wapi ktk biblia?? Umeongeza mwenyewe au?
Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu anatufunuliwa wahusika au mawakala watano
ambao ni:
1—Mnyama mwekundu wa Ufunuo 12—Shetani mwenyewe
2—Mnyama mfano wa chui wa Ufunuo 13—Rumi ya kidini
3—Mnyama mfano wa mwana kondoo wa Ufunuo 13:11—Taifa la Marekani
4—Sanamu ya Mnyama Ufunuo 13—Umoja wa makanisa —WCC
5—Mnyama wa rangi nyekundu sana na mwanamke wa Ufunuo 17—-Illuminati,
freemason wakiwa wameungana na kanisa la Rumi..

TWENDE SASA TUWAONE FREEMASON NA ILLUMINAT KWENYE UFUNUO


Wengi hawakuwa wanatofautisha wanyama hao lakini utakapojifunza kwa undani
zaidi utagundua kwamba mnyama wa Ufunuo 17 ambaye ni mwekundu sana mwenye
pembe kumi na vichwa saba ambaye amembeba mwanamke inamaanisha muungano wa
Illuminati wakiwa wameunda majimbo kumi katika dunia nzima pamoja na kanisa la
Rumi likiwa na watawala saba tangu kuanza kazi yake baada ya kupata jeraha la mauti.

Biblia inapotumia neno mwanamke kiunabii humaanisha kanisa (Ufunuo 21:2) na neno
‘kichwa’ humaanisha kiongozi wa kanisa ambapo kwa kanisa la Mungu, kichwa ni Kristo
lakini kwa kanisa la uongo, kichwa ni mwanadamu aliyechukua nafasi ya Yesu duniani,
(Wakolosai 1:18; 2Wathesalonike 2:4).

Biblia kamwe haijawahi kutumia neno ‘kichwa’ kumaanisha kiongozi wa kiserikali ila hutumia neno ‘watawala au wafalme’. Ndio maana vichwa saba inamaanisha vipindi saba .

Ufunuo 17:8 anasema kwamba mnyama huyo yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na
katika

Ufunuo 9:11 tunasoma kwamba “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa
kuzimu…”.


Aya zote hizo zinamaanisha umizimu (spiritualism) ambayo ni imani
ya Illuminati. Imani hii inamfanya muumini aamini kwamba hakuna kifo na mtu
anapokufa anakuwa amebadilisha mahali kwa kuhama duniani na kwenda mahali pengine
akiendelea kuishi na kwamba hiyo ndiyo mbingu yake maana hawaamini kama kuna
ufufuo.

Chanzo cha fundisho hili ni Shetani alipomfundisha Hawa kwamba “Hakika
hamtakufa” Mwanzo 3:4.


Hivyo tutajifunza na kuona ukweli huu wa Illuminati kwa
kujiunga na kanisa ili kutimiza malengo yao.

wahusika wa hayo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa siri kubwa kiasi cha kuwafanya watu
mamilioni wasielewe kinachoendelea

“The great strength of our order lies in its concealment,” yaani “nguvu kubwa ya
utaratibu wetu iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa” ni maneno ya
Adam Weishaupt, mwanzilishi wa Illuminati mwaka 1776. Akaendelea kusema, “Let it
never appear in any place in its own name, but always covered by another name and
another occupation” yaani “Hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima
ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine.” (Kutoka kwa Robin’s Proofs of a
Conspiracy, p. 195.)
 
Nashukuru Sana kwa ufafanuzi mzuri ngoja pakuche ndio nipitie tena. Wasi wasi wangu ni kwanini biblia haitaji moja kwa moja majinw haya kiasi kwamba Msomaji analazimika kusoma historia ya dunia na jiogragi kali tena ya ndani sana ili kuelewa huo unabii? Je hili halitoi mwanya kwa wasomaji wenginr kutafsiri kadri wanavyoona wao kama ulivyofanya?
 
KESHO NITAKUELEZA KWANINI DANIEL NA UFUNUO VIMEANDIKWA KWA CODE
 
Duuh shule ngumu sana hii. Ngoja nitulize kichwa kwanza. Anyway hata hivyo mimi ni mfuasi wako kule youtube masomo yako ni haya haya.
 
Freemason sio mfumo wa nguvu za giza na haulingani kwa namna yoyote na uganga wa kienyeji
Freemason ni mfumo Tu wa nguvu za Giza uliopo ulaya , huku tuna mfumo wetu wa waganga wa kienyeji, mmiliki Yule Yule kaya tofauti , na waliostarabika zaidi basi freemason wanachukua nafasi , Dunia ni ya Mungu Ila shetani ndo mkuu wa dunia hii .....
 
Nondo tupu ila Freemasons au wajenzi huru hawajiusishi na siasa wala dini yoyote,ni moja kati ya torati zao.
Pasipo mfumo wa siasa itakuwa njia ndefu wao kufanikisha hazima yao, unapaswa kujua hii siasa wanaitumia kufikia lengo la kuja kutawala dunia...
 
Msabato kwenye ubora wake mnamtaja mpinga kristo wakati ndio nyie wenyewe ao wengine mnawapakaza damu mseme wameumia kumbe ni damu zenu wenyewe...Ellen alianzisha nyie malizieni kutoa kashfa
 

Usabato Ni laana kwa ulimwengu
 
Mnyama wa ufunuo mwenye vichwa Saba ni rumi, ufunuo ni muendelezo wa kitabu Cha Daniel mnyama wa nne wa Daniel mwenye pembe 10, na mnyama wa ufunuo mwenye pembe 10 na vichwa 7 ambazo ni milima Saba ulipojengwa mji wa Roma.

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
mimi kinachonitatiza hiyo milima saba imeandikqa wapi kwenye ufunuo? isiwe ikawa ni binadamu tunaongeza maneno na tafsi zetu maana Biblia inatakiwa ijitafsiri yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…