Ubarikiwe sana mkuuGharama za ushuru ziko wazi sana mkuu, link hapa chini itakusaidia kujua kodi ya gari utakayopaswa kulipa kabla haujafanya maamuzi ya kununua gari nje ya nchi.
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
Gharama za ushuru ziko wazi sana mkuu, link hapa chini itakusaidia kujua kodi ya gari utakayopaswa kulipa kabla haujafanya maamuzi ya kununua gari nje ya nchi.
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
Nataka niagize music system ni vitu gani napaswa kuwa navyokaribu sana mkuu, unaweza kututumia sisi.
1.Gharama za wakala wa meli (shipping line) ni $85 (Delivery Order fee, sumatra charges, car service charges) VAT included.Nashukuru sana kwa msaada wako. Mfano, gari inauzwa USD 2500 na valuation lets say million 4 tsh.
Vipi tena kuhusu gharama zingine kama shipping na kuitoa bandarini. Naweza juaje hizo gharama pia. Ili niwe najumlisha mchakato mzima ili nipime uwezo wangu.
Nisaidie nijue from point one mpaka mwisho wa mchakato mpaka inakaa mkononi. Barikiwa sana kwa response yako.
Zachaja,1.Gharama za wakala wa meli (shipping line) ni $85 (Delivery Order fee, sumatra charges, car service charges) VAT included.
2.Gharama za bandari;
a). Handling charges, ambayo rate yake ni $7 plus VAT per CBM (Cubic Measurement yaani Urefu x Upana x Urefu). mfano Toyota IST ina CBM 10.12, kwa hiyo handling charges: (10.12 x $7) + VAT = $83.59
b). Corridor Levy, ambayo rate yake ni $0.3 plus VAT per CBM, mfano kwa IST inakua: (10.12 x $0.3) + VAT =$3.59
c). Wharfage charges, ambayo kwa sasa TRA wanaikusanya kwa niaba ya Bandari, rate ya wharfage ni 1.6% ya C.I.F value plus VAT. mfano Toyota IST yenye C.I.F $ 2,235, wharfage charges: ($2,235 X 1.6%) + VAT =$42.20.
3. Mwisho mkuu ni gharama za uwakala (agency fee) inaanzia laki mbili (200,000) na kuendelea.
A: Gharama za bandari utalipa kiasi kisichozidi;Zachaja,
Mimi nina Toyota ISIS ya 2008, 1800cc ambayo inakuja karibuni. Hivi gharama za bandari na shipping line zinaweza kuwa kama shilingi ngapi?
Samahani mkuuMkuu ushuru wa scania mende ( 8x4 Rigid 26 to 32 tonnes) inategemea ni mwaka gani, mfano scania mende ya mwaka 2000 ushuru ni $18,524.75 (tsh.42,412,407.69) na mende ya mwaka 1997 ushuru ni $15,884.48 (tsh. 36,445,902.39) hii ni kama inavyoonyesha kwenye TRA calculator.
Ubarikiwe.Gharama za ushuru ziko wazi sana mkuu, link hapa chini itakusaidia kujua kodi ya gari utakayopaswa kulipa kabla haujafanya maamuzi ya kununua gari nje ya nchi.
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
Kupitia link hii Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System unaweza kujua kiasi cha jumla ya kodi unayopaswa kulipa kabla gari halijaingia nchini. Ukifungua hiyo link unachagua MAKE (mtengenezaji wa hiyo gari mfano Toyota), unachagua MODEL & BODY mfano Harrier, unachagua YEAR OF MANUFACTURE (mwaka wa gari kutengenezwa) mfano 2002, unachagua COUNTRY OF ORIGIN (nchi gari ilikotengenezwa) mfano Japan, unachagua FUEL TYPE (aina ya mafuta gari inayotumia) mfano Petrol, pia unachagua ENGINE (ukubwa wa engine ya gari) mfano 2001-2500cc. Mwisho unabonyeza CALCULATE utapata jumla ya kodi utakayopaswa kulipa katika Dollar na katika shillingi, ingawa katika shillingi, kiasi kitakua kinabadilika badilika kutegemeana na kupanda au kushuka kwa Dollar dhidi ya shillingi.Samahani mkuu
hiyo tra calculator inakuaje?
natamani kifahamu iyo formular ili niitumie kujitathmini kama nitaweza kumudu gharama za gari ninayotaka kugiza kupitia befoward. Tafadhali nisaidie
Karibu sana mkuu, tunafanya kazi kwa ufanisi, uaminifu mkubwa na kwa bei nzuri.Mkuu nimeshachkua namba zenu
Kwa kweli mtanirahisishia saaana kazi manake huwa napitishia mizigo mara kwa mara kwa agent wa ZNZ inachkua muda saaana kunifikia na gharama zao zipo juu
Karibu sana mkuu, tunafanya kazi kwa ufanisi, uaminifu mkubwa na kwa bei nzuri.
Mkuu unaposema hizo taarifa itakusaidia kujua gharama za kodi as per TRA Calculator....kivipi wakati TRA Calculator hairuhusu wewe kuingiza moja ya taarifa hapo juu yaani gharama Halisi za gari(Invoice) ila ni taarifa nyingine tuu.Mkuu karibu utupe kazi ya ku-clear gari yako tunafanya kazi kwa ufanisi, haraka na kwa bei nzuri, gharama zetu (agency fee) tutakutoza shillingi laki mbili tu (200,000).
Ili mzigo usipate gharama za storage utatakiwa utukabidhi nakala (copy) za document za mzigo husika siku saba (7) kabla ya gari kuwasili bandarini. Document hizo ni Bill of Lading, Invoice, packing list na cheti cha ukaguzi (motor vehicle inspection certificate). Hii itasaidia kujua gharama za kodi/ushuru (as per TRA calculator), gharama za bandari (handling charges) na pia gharama za wakala wa meli (shipping line).
Karibu sana mkuu.
Ni kweli mkuu, lakini invoice value inatusaidia kujua ushuru wa gati ( wharfage ), pia itatusaidia kulinganisha CIF value (gharama ya gari + bima + usafiri ) ya kwenye TRA calculator na ya kwenye invoice, hivyo kumshauri mteja apate invoice ilio sawa au chini ya TRA CIF value. Kwa mfano, IST ya 2005 mteja ameleta invoice ya Dollar 3,144 lakini kwenye TRA calculator ni Dollar 1,789, kwa hiyo mteja atashauriwa aombe invoice nyingine "for customs purpose" ambayo itakua chini kidogo ya $1,789.Mkuu unaposema hizo taarifa itakusaidia kujua gharama za kodi as per TRA Calculator....kivipi wakati TRA Calculator hairuhusu wewe kuingiza moja ya taarifa hapo juu yaani gharama Halisi za gari(Invoice) ila ni taarifa nyingine tuu.