Fridge/Freezer

Click Hapa

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
479
Reaction score
206
Habari za jioni Wadau!

Miye ni Mjasiriamali nipo Mwanza, ktk pitapita zangu huku na huko kusaka fursa nimepita center moja huko vijijini imechangamka kweli, kwa kuwa ilikuwa mchana na kajua kalikuwa kamewaka ka kutosha ikabidi nile pozi sehemu ili angalau nipate soda au juice baridi, nilipouliza tu nikaambiwa vinywaji vilivyopo ni vya moto kwa kuwa center hiyo haina umeme, hapo hapo nikawa nimeiona fursa ya kuuza cold drinks center ile na kwa jinsi palivyochangamka najua nita-make tu.
Sasa naomba kwa yeyote mwenye kujua anisaidie ni wapi nitapata zile Fridge ama Freezer zinazotumia mafuta ya taa, na je ni bei gani zinauzwa na kwa size gani.

Mniwie radhi kwa maelezo marefu nimeyaeleza haya yote ili kuweka mambo sawa.

Natanguliza shukurani.
 
Mkuu kwa uzoefu wangu fanya hivi, tafuta frem ya biashara funga sola nunua friji ya sola kwa maana inayotumia 12v dc na bulb pia utapata mwanga na simu utachajisha anza biashara!
 
usipate tabu ongea na coca cola na pepsi wote watakupa fridge uza soda zao kwa mkataba maalyumu
 
Sikuwah kujua kama kuna friji inatumia mafuta ya taa
 
Mkuu shukurani kwa ushauri, sasa hizi fridge za solar zinapatikana wapi? Waweza kunipa contact za dealers?
 
Friji ya mafuta ya taa ni old fashion na kwa sasa hazipo tena. Ni frji ambazo zinatumia gas aina ya ammonia ambayo si nzuri kiafya na mazingira. Ambapo mafuta ya taa hutumika ku heat ammonia. Baadae walitoka kwenye mafuta ya taa na mbadala wake wakatumia heater ambako ulikuwa unachomeka kwenye umeme. Lakini gas ya ammonia haitumiki tena kwenye industry ya refrigeration na AC badala yake inatumika R 600a R 134a na zingnezo na hata R 12 nayo imepigwa marufuku.
Cha muhimu ni kutafuta solar kama alivyosema mdau.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mkuu shukurani kwa ushauri, sasa hizi fridge za solar zinapatikana wapi? Waweza kunipa contact za dealers?

Zara Enterprise; wako karibu na Msikiti wa Ijumaa; ndo magwiji kwa huduma za Solar
 
msikiti wa ijumaa uko maeneo gani?

Siju nianzie wapi kukuelekeza ....
Kati ya sehemu hizi ni ipi unaijua?
1. Soko kuu Mwanza karibu na stand ya tax / daladala
2. Barabara ya Nyerere karibu na duka la semira,
3. Stanbic bank ....
nasubiri majibu yako nikupe maelekezo ...
 
Siju nianzie wapi kukuelekeza ....
Kati ya sehemu hizi ni ipi unaijua?
1. Soko kuu Mwanza karibu na stand ya tax / daladala
2. Barabara ya Nyerere karibu na duka la semira,
3. Stanbic bank ....
nasubiri majibu yako nikupe maelekezo ...

mi niko dar
 

Mkuu nashukuru sana kwa ushauri huu, actually nilienda kwenye option hii baada ya kuona Coca cola bado wanazo fridge za aina hii na zinatumika sana vijijini, tatizo lao ni kwamba wana restrictions sana, wao hawataki wakute umeweka bidhaa tofauti na products zao, hivyo nikaone nishirikishe wana jamvi kuona kama kuna uwezekano wa kupata fridge iliyo free/multipurpose. Asante kwa ushauri once again.
 
Zara Enterprise; wako karibu na Msikiti wa Ijumaa; ndo magwiji kwa huduma za Solar

Asante mkuu kwa maelekezo haya, napafahamu vizuri sana Zara Entp. Kwa kuwa nipo Mza hapahapa nitaenda kuwaona. Thanks sana.
 
karne ya 21 ,unaulizia friji ya mafuta ya taa?

Mkuu unashangaa nini hapo, hivi hujui Tanzania hii bado kuna watu wakiona Gari wanakimbia mbaya? Mkuu kwa taharifa yako kama wewe unaishi mjini kuna maeneo nchi hii watakushangaa wakiona unalalamika eti bei ya umeme imepanda, wao ukitaka ukorofishane nao pandisha bei ya chumvi, mafuta ya taa na mengine yanayofanana na bidhaa hizo.
Kwa kifupi wewe unazungumzia karne ya 21, Tanzania bado kuna WAJIMA, unakumbuka enzi za UJIMA ilikuwa karne ya ngapi??? Pole sana mkuu TEMBEA UONE.
 
mi niko dar

Watoto wa MJINI bwn, yaani hamjui kabisa mambo yanavyokwenda huku. Hali ni mbaya mkuu usikae Dar ukadhani nchi nzima ni kama Dar. Huku kuna watu hata hawajui kama Mwl. Nyerere alishakufa.
 
Duuh kuna friji za mafuta ya taa?? Hii kwangu mpya
 
Duuh kuna friji za mafuta ya taa?? Hii kwangu mpya

Zipo, huwa zimetengenezwa special kwa maeneo ya vijijini ambapo hakuna umeme ila siku hizi zimekuwa hazipatikani kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…