Friendly match: Simba sc vs African sports

Friendly match: Simba sc vs African sports

WanaSimba wenzangu tukubali kwamba huyu Bwalya tulilizwa na Senzo anazidiwa na Mukoko mbali mnooo, siyo mpambanaji Uwanjani. Ana mpira ule ule aliokuwa nao Shiboub, mara elfu 1 tungeendelea na Shiboub kuliko huyu konokono Bwalya. Hana ubunifu wa kuisaidia timu, halafu nashangaa kocha anamwacha nje Kahata anamchezesha huyu Bwalya. Anyway mim binafsi sijamuelewa kabisa, wale mliomwelewa mnisamehe.
Kahata pole sana kwa masaibu unayopitia lkn wakat utaongea
Ilikuwa awe Mwananchi lakini mkamuwahi. Kuleni faida yake
 
Mi huwa najiuliza,Hivi Simba huwa inadanganywa na nani katika kusajili na kuajiri mwalimu wa timu?

Mbona wenzetu wanajitahidi sana hata kipindi walichokuwa wakilia njaa timu haikuyumba sana?
 
Kwangu Mimi, shiboub alikuwa na umuhimu kuliko bwalya. Tatizo kubwa la bwalya Hana killing instincts, yaani anacheza Kama yuko mazoezini hatuko sharp, anageukia nyuma Kila wakati na Kila mpira anaoupata anataka kupaka rangi au kulazimisha kuucheza kwa mbwembwe

HUYU mchezaji anababisha timu yetu ikose kasi wakati wa kwenda mbele na ndiyo maana Kila Simba inapotaka kwenda mbele tunakuta wapinzani washakuwa wengi kwasababu yake

Lakini hili tatizo kocha anao uwezo wa kumbadili ili awe na pasi za haraka na kamwe chaguo lake la kwanza lisiwe kigeukia golini kwetu anapopata mpira

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
Jana Zambia National Team walicheza bila kina Bwalya na Chama, ina maana hawa wachezaji hawako National Team?
 
IMG-20201116-WA0027.jpg
 
WanaSimba wenzangu tukubali kwamba huyu Bwalya tulilizwa na Senzo anazidiwa na Mukoko mbali mnooo, siyo mpambanaji Uwanjani. Ana mpira ule ule aliokuwa nao Shiboub, mara elfu 1 tungeendelea na Shiboub kuliko huyu konokono Bwalya. Hana ubunifu wa kuisaidia timu, halafu nashangaa kocha anamwacha nje Kahata anamchezesha huyu Bwalya. Anyway mim binafsi sijamuelewa kabisa, wale mliomwelewa mnisamehe.
Kahata pole sana kwa masaibu unayopitia lkn wakat utaongea
Watasema msaliti au wewe Mwananchi,maana huwa hawakubali kukosolewa......kumbe ndiyo ukweli.......
 
Huwa wanacheza vzr wakicheza na Gwambina na Ihefu, mechi kubwa hawaziwezi,sio rahisi wao kuitwa National team.
Nilifikiri akiitwa "Mwamba wa Lusaka" means Lusaka yote wanamjua au wanamkubali.
 
Back
Top Bottom