Friends of Simba kubalini matokeo kwa maslahi ya Simba, vinginevyo Yanga wapewe kombe lao mapema

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Zipo taarifa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya kundi la Friends of Simba kuhusu viongozi waliochaguliwa, wapo waliosema wanaunga mkono viongozi anaowataka mwekezaji na wengine wanaona maslahi yao yanapotea hivyo wanataka kupandikiza watu wao ili maisha yaende.

Zipo taarifa mbaya hata gemu na Dodoma FC tuliyoshinda kwa bao 1 0 baadhi yao walikutana usiku kutengeneza mazingira tupoteze mchezo ule, kwa kweli najiuliza kama kweli hawa ni wapenzi na wanachama wa Simba, haya maelezo sio yangu ameyatoa Hassan Hassanoo Mpiganaji wakati akiongea na wanachama wa Simba pale Dodoma.

MO DEwji aliweka masharti kwa uongozi kuwa fulani na fulani ndio anawahitaji mwenye uongozi, wasiposhinda hao hawezi kuingiza mpunga wake, sasa kuna gogoro linafukuta na kuna tetesi mechi na Singida tutapigishwa shoti sio ya nchi hii ili tu Mangungu aonekane hafai.

Sio vzr ndugu friends of Simba, mnawakosesha usingizi wanachama, mashabiki na wapenzi.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimechukizwa Mangungu kurudishwa tena madarakani,ana makando kando mengi sana,ila siungi mkono hujuma kwa timu kwani itawaumiza mamilioni ya wanachama na washabiki. Waliomchagua tena huyu kilaza wameshatuumiza sasa si vema tukaendelea kuumizwa tena na Friends of Simba, watafute njia nyingine ya ku challenge hayo matokeo kisheria.
 
Yaani mmeletewa Manzoki na yeye Manzoki kutamka Hadharani apa Africa anapenda Simba tu bado hamtosheki, Basi uchaguzi ujao tutawaletea Mess labda mta poa.
 
Bigirimana alisajiliwa na yanga akuletwa kufanya show off kama manzoki, Tuambieni uyo manzoki mmemsajili lini na yeye ni nani ndani ya simba mpaka alipiwe nauli kuja kudanganya watu?
Hata RC Amos Makala alialikwa. Je, alikuja kudanganya watu?
 
Mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine anapistiwa kwenye page rasmi za klabu nyingine very unproffesional!!
pole aisee, ndio ameshahudhuria hivyo, tena akawaita manyoka nyoka
 
Hata friends of Simba wakikubaliana, msimu huu Yanga Bingwa,acheni kutafuta sababu ya kupoteza ubingwa msimu huu tena......
 
Bigirimana alisajiliwa na yanga akuletwa kufanya show off kama manzoki, Tuambieni uyo manzoki mmemsajili lini na yeye ni nani ndani ya simba mpaka alipiwe nauli kuja kudanganya watu?
Mashabiki wa Simba wamepewa Ugali na Picha ya Samaki,nizaidi ya dharau kwao
 
Mo ni kanjanja anajua wakiingia wapya watadai ile 20bn hivyo anahitaji mipang'ang'a ili arndelee kutupiga wana simba mikia.
 
Hata RC Amos Makala alialikwa. Je, alikuja kudanganya watu?
Rc kaalikwa sababu ya cheo chake,Sasa Manzoki yeye alikuja kama nani pale kwenye mkutano wa Simba nafikiri hizi ni siasa tu za mpira zisizokua na faida yoyote bali kutaka kufanya watu kua ni wajinga tu..
 
Rc kaalikwa sababu ya cheo chake,Sasa Manzoki yeye alikuja kama nani pale kwenye mkutano wa Simba nafikiri hizi ni siasa tu za mpira zisizokua na faida yoyote bali kutaka kufanya watu kua ni wajinga tu..
Labda tuanze kwa kujiuliza, Je, katika wale wagombea, kuna yeyote aliyedai au aliyedaiwa kuwa amemleta Manzoki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…