Friji inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa mke nyumbani?

Friji inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa mke nyumbani?

Wakuu, nimejibana nimepata shilingi 1million mke wangu amenishauri nimemnunulie friji kuanzia laki 5-8 pesa itakayo baki laki 2 afanye kama mtaji wa kuuza barafu, Ice cream na juice. Naomba ushauri wenu je hii biashara inaweza inaweza zaa matunda na kurudisha hiyo pesa? Natanguliza shukrani.
Italipa vizuri tu kama huyo mlengwa atakuwa sehemu ambayo kuna wateha wa hivyo vitu, yeye ni mchakalikaji yaani kutafuta wateja na vile vile yupo around muda anapohitajika. Pamoja na Friji mnunulie cool box ili kama anapata mtu wakumzungushia, anakuwa natoa juice in the morning then someone can pass through places where people normaly have mitoli na soup wanaweza kununua na juice mradi iwe original siyo za kopo. Mnunulie na blender ya kutengeneza juice au mixer. You wont regret.

Nasema hivi nina mdogo wangu anasomesha watoto sababu ya hii kitu ingawa ana na kigenge nje ya gate.
 
Wakuu, nimejibana nimepata shilingi 1million mke wangu amenishauri nimemnunulie friji kuanzia laki 5-8 pesa itakayo baki laki 2 afanye kama mtaji wa kuuza barafu, Ice cream na juice. Naomba ushauri wenu je hii biashara inaweza inaweza zaa matunda na kurudisha hiyo pesa? Natanguliza shukrani.
Yes iko poa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, naona sasa umeamua kunizibia riziki humu, mimi ndo kwanza mwakani naingia kidato cha 2.

Napenda sana mwanamke anayejiongeza kama mke wa mleta mada, ndio maana nampigia debe proposal yake ipitishwe na mwezeshaji wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata usijali 'serengeti boy wangu' riziki yako ya kung'oa watoto wakali wa JF mwaka 2019 iko pale pale maana wanajua fika kuwa nakutania wewe ungali mwanafunzi wa darasa la 7 'D'

Hakika huyo mwanamama amejiongeza kuliko kukaa kibarazani na kupaka hina huku akipiga umbea atakuwa anakaa zake kibarazani akifunga ice-cream na marafu yatakayo iongezea kipato familia yake.
 
Back
Top Bottom