Friji inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa mke nyumbani?

Friji inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa mke nyumbani?

Hata usijali 'serengeti boy wangu' riziki yako ya kung'oa watoto wakali wa JF mwaka 2019 iko pale pale maana wanajua fika kuwa nakutania wewe ungali mwanafunzi wa darasa la 7 'D'

Hakika huyo mwanamama amejiongeza kuliko kukaa kibarazani na kupaka hina huku akipiga umbea atakuwa anakaa zake kibarazani akifunga ice-cream na marafu yatakayo iongezea kipato familia yake.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Huku ndo kunaitwa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.

Hakika amepata mke mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wazo zuri hilo la Biashara. Pia hutegemea na aina ya wateja wanaowazunguka. Mfano kama mnakaa karibu na bahari - wauza samaki watakuwa wateja wenu wakubwa wa mabarafu. Au kama mpo karibu na shule ya msingi - mtapata wateja wengi wa ice cream. Chamsingi kabla ya kuanzisha biashara fikiria kwanza na soko la bidhaa zako lazima utatoboa.
 
Italipa vizuri tu kama huyo mlengwa atakuwa sehemu ambayo kuna wateha wa hivyo vitu, yeye ni mchakalikaji yaani kutafuta wateja na vile vile yupo around muda anapohitajika. Pamoja na Friji mnunulie cool box ili kama anapata mtu wakumzungushia, anakuwa natoa juice in the morning then someone can pass through places where people normaly have mitoli na soup wanaweza kununua na juice mradi iwe original siyo za kopo. Mnunulie na blender ya kutengeneza juice au mixer. You wont regret.

Nasema hivi nina mdogo wangu anasomesha watoto sababu ya hii kitu ingawa ana na kigenge nje ya gate.

Nakushukuru sana Mkuu, tayari nimemnunulia brenda aina ya Philips mpya 800W, na hii brenda ndio imempa sana hamasa na hii biashara aliamua kubuni maana huhitaji wa bidhaa hizo hasa barafu ni mkubwa sana na sikuweza kufikiria hilo kwa kuwa friji nilalotumia ni la kupooza tu.
 
Ni wazo zuri hilo la Biashara. Pia hutegemea na aina ya wateja wanaowazunguka. Mfano kama mnakaa karibu na bahari - wauza samaki watakuwa wateja wenu wakubwa wa mabarafu. Au kama mpo karibu na shule ya msingi - mtapata wateja wengi wa ice cream. Chamsingi kabla ya kuanzisha biashara fikiria kwanza na soko la bidhaa zako lazima utatoboa.
Ndio Mkuu, tuko jirani sana na bahari. Unaonaje nikichukua friza badala ya friji ambalo ni la kawaida lenye freezer na sehemu ya kupooza yaani (friji)
 
Inalipa Bila Shaka
Mimi Nilinunua Dogo Mpaka Sasa Ana Millions 1.3
Hiyo Itakulipa Punde
 
Ukianza kuona elfu kumi inakuja kununua ashikirimu iwekee umakini sana hela za barafu zinajulikana maana itakosekana jenji atafata dukani atafatwa nyuma nyuma na kuombwa namba na kuambiwa keep chenji barafu anaramba inaisha wew umebaki sebleni na fridge linakuungurumia hapo

Sent from my TECNO K7 using Tapatalk
 
Hahaha huku dar
Sasa baby niandike mipango yangu hapa jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo hujawahi hata kujifunza au kujishikiza kwa mtu kwenye hii biashara,

Mi nilitaka nifungue mghahawa wa kisasa, sema sina uzoefu na usimamiz ndo mzk....

Ulinishawishi wazo lako, sema na ww upo km mm.....

At least ungekuwa na uzoefu nayo tungeingia partnership

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom