Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Ni mchuano wa kufuzu kwenye fainali za AFCON za mwaka 1980 ambapo Taifa Stars ilikua inacheza mchezo wa marudiano na Zambia mjini Lusaka. Stars walihitaji goli moja tu waeze kufuzu
Peter Tino alipokea pass ya counter attack akiwa katikati ya uwanja kwenye duara la kuanzishia mpira. Akawa ana dribble kwa kasi kuelekea langoni mwa KK Eleven Boys. Akataka kupiga shuti akiwa mbali kidogo na goli.
Kocha wakati huo marehemu Joel Nkaya Bendera akasimama na akawa ana shout huku kakinga mikono mdomoni ili sauti imfikie Peter Tino. Kila Tino akitaka kupiga Bendera anamwambia "Tino baadoo", Peter Tino ana dribble, akataka kupiga tena, Bendera "Tino baadooo" jamaa aka dribble huku anasepa na kijiji cha mabeki wa adui, akataka kupiga tena kwa mara ya tatu Bendera aka shout " Tino Baadoo" Peter Tino akaendelea na dribbling na juggling zake
Peter Tino akawa ameingia sasa kwenye semi circle na bado mpira upo kwenye control yake. Coach Joel Bendera aka shout tena maelekezo....."Tino piiiigaaaa" Sekunde ileile Peter Tino akaachia block buster ambapo mpira ulikwenda kuingia golini kwenye nyuzi 90 ukapitiliza juu kwenye nyavu na ukatua kule anakotagia kuku huku ukimuacha kipa Vicent Chileche wa Zambia akigaagaa chini asijue la kufanya!
Mtangazaji wa Radio Tanzania wakati huo alikua "Faza" Ahmed Jongo na alishindwa kabisa kusema goooo, akawa amepagawa huku anasema "Laagoooos, Laagoooos, Laagoooos, Laagooos, Laagoooos" Na ndivyo ilivyokua Taifa Stars ikafuzu kucheza fainali za soka Za Mataifa Huru ya Afrika kwa mara ya mwanzo na ya mwisho zilizofanyika Lagos Nigeria 1980!