Fructose sweet, but dangerous

Fructose sweet, but dangerous

damian marijani

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2010
Posts
695
Reaction score
466
Leo nataka nitoe mada hii kuhusu fructose. Hii ni aina ya sukari inayopatikana kwenye matunda mbalimbali. Kwa kawaida kuna aina tatu kuu za sukari (simple sugar au monosaccharides) nazo ni: glucose, fructose na galactose (inayopatikana kwenye maziwa).
Fructose inapoliwa haisababishi kupanda kwa sukari katika damu kwa sababu inabidi iwe processed kwenye ini iweze kugeuzwa kuwa glucose. Glucose ndiyo sukari pekee ambayo mwili unaitumia katika viungo mbalimbali kama source of energy. Hivyo basi fructose imekuwa ikitajwa kuwa ni moja ya vyakula vyenye Low glcemic index.
Kwa maelezo hayo hapo juu itaonekana kuwa fructose ni nzuri kuliwa. Hapa nataka kutoa angalizo kuwa sukari hiii inapoliwa kwa kiasi kidogo haina tabu. Lakini inapoliwa kwa kiasi kikubwa ina madhara makubwa.
Baadhi ya madhara hayo ni kama:
Kuwa na mafuta (triglycerides) kwenye mzunguko wa damu. Hii inatokana na kushindwa kwa ini kuprocess fructose wakati inapoliwa kwa wingi. hivyo ini linatengeneza mafuta aina ya Triglycerides ambayo yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo.
Fructose inaweza kusababisha kuongeza hamu ya kula (appetite) kwa ajili ya kutoweza kuongeza glucose kwenye damu katika kipindi kifupi kama ilivyoelezwa hapo juu.
Matumizi ya fructose kwa wingi inaweza kusababisha kuwa na ugonjwa wa kisukari.
 
Hujatuweka bayana matunda hayo yenye hiyo fructose ni yapi,au kila aina ya tunda?
 
Mkuu, swali zuri. Matunda na mbogamboga nyingi yana kiwango kidogo cha fructose ambayo mwili unaweza kuhandle bila ya madhara. Shida ipo kwenye High frucose corn syrup ambayo ina 55% fructose na 45% glucose. Nitakupa mifano hai ya viwango vya fructose: Nyanya zilizokatwakatwa zikijaa kikombe chai zina 2.5g ya fructose, soda ya nusu litre ina 62g ya fructose. Asali nayo ina 50% fructose na glucose.
 
Asali sio mbaya kwani mara nyingi hutumika kama dawa hivyo hailiwi kwa wingi kama ukilinganisha na vitu kama soda unaweza ukabugia kwa wingi bila kujua umeweka nini tumboni mwako.
 
Aisee somo zuri. Sasa soda tushajua ni mbaya, kila mahali unakutana na hilo jambo. Naomba utuambie vitu gani ambavyo vina high fructose, ambavyo watu wanakula lakini hawajui hilo. Asante.
 
Back
Top Bottom