FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Stade de L' amitie General

FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Stade de L' amitie General

Sio mtaalamu wa soka lakini nikionacho mara zote Simba wanakawia sana kustukiza mashambulizi.

Wanafika golini kwa adui kisha wanasubiri adui ajipange ndio waanze sambusa zao goli kupatikana ni 1/10.

Wanafika golini au jirani na goli hata mita 20 hawa shoot. Wanataka kuingia na mpira langoni.

Ona magoli yaliyofungwa na Asec yote ni mita za kutosha na hakuna wa kuremba. Swali Simba wajiulize hawawezi ku geuka na ku shoot?

Naona watu pale mbele kuanguka anguka tu. Kibu akipokea pasi mara zote ataanguka tu. Boko vivyo hivyo. Kocha haoni hayo?

Ningetamani kuona Mkude na Bwalya wana shoot kila mmoja angalao mara 5 hata wakikosa wanajaribu. Wafanyie mazoezi jambo hilo.

Ningetamani kuona beki Mohamed ajifunze kwa Enock namna ya kuzuia washambuliaji matata anaweza sana.

Usajili ujao Simba isajili wabunifu pale mbele. Kongole kwa Morrison anaonesha umahiri na akili kubwa ya mpira.

Nimeumia lakini Simba bado ni timu nzuri irekenishe mapungufu.
Hili kundi hata tukivuka robo huko mbele hatutoboi,game za ugenini at least kocha Gomez aliyeondoka aliweza kidogo japo mechi ya kaizer kule south ilimuharibia,hii inaonesha kuwa kuna matatizo haswa upande wa back line huwa hayarekebishwi,tutazidi kupigwa goli nyingi hadi watu wa usajili wabadilike,kingine japo sina utaalamu sana wa football ila naona Simba hawana mtu wa saikolojia mechi za ugenini confidence yote ya wachezaji huwa inapotea,baada ya hapo ni goli tu huwa zinaingia tatizo nini?,yote kwa yote katika dirisha la usajili msimu huu tulibahatika kupata wachezaji wawili tu wa maana Sakho na inonga basi,viongozi tunaomba watu kama kagere, kanoute au lwanga,mugalu,Wawa,bwallya na onyango watupishe tusajili wengine bila hivyo hakuna tutakachofanya.
 
hajui soka la kiafrica huyu anaendeshwa na mihemko .soka la Africa sio kama la ulaya ambalo timu iwe home iwe away winning chance bado itategemea na mwenye uwezo. lakini Africa ni tofauti ,yani Africa ni kama vile ukiwa home tayari una goli moja mkononi.
Embu niambia ni advantage ipi hiyo inayombeba mwenyeji kwa Africa? ni uchawi? Au ni Rushwa au mbinu zipi za nje ya uwanja?

Wiki hii tumeshuhudia Raja Casablanca, Al Ahly, Mamelod, whydad, Es Tunis wkishinda ugenini
 
Timu ngapi zinatakiwa kuvuka kwa kila kundi,isije nikajipa matumaini yasiyokuwepo...
 
hajui soka la kiafrica huyu anaendeshwa na mihemko .soka la Africa sio kama la ulaya ambalo timu iwe home iwe away winning chance bado itategemea na mwenye uwezo. lakini Africa ni tofauti ,yani Africa ni kama vile ukiwa home tayari una goli moja mkononi.
yaan timu ikifungwa home kama muujiza hv
 
Back
Top Bottom