FT: Azam FC 1-0 Simba SC | NBC League, 28/10/2022

FT: Azam FC 1-0 Simba SC | NBC League, 28/10/2022

Pettymagambo

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2017
Posts
1,490
Reaction score
8,227
Ni bandika bandua leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, pale miamba ya soka Afrika mnyama mkali mwituni wekundu wa msimbazi, watakapo karibishwa na matajiri wa Azam FC katika kuwania pointi 3 muhimu ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu!

Mara baada ya mnyama kutoshana nguvu na mtani wake wa jadi Jumapili iliyopita na azam kukung'utwa 2-1 na KMC, leo watapata nafasi ya kujiuliza,
ngoma ni saa 1 kamili jioni hii!

Wanalunyasi karibuni, mwana kulitaka mwana kulipewa.

Nguvu moja.

=======

01' Mpira umeanza Benjamin Mkapa.

08' Ayoub Lyanga anajaribu kutoka nje ya 18 lakini mpira unapaa juu ya lango la Simba.

13' Kyombooooo, anakosa bao baada ya pasi nzuri kutoka kwa Okra.

17' Azam wanafika kwenye lango la Simba, Kona. Simba wanasimama imara na kona haina madhara..

22' Simba wanacheza pasi nyingi kuelekea lango la azam, mikono ya Ahmada inawaokoa Azam.

23' Onyango anamdhibiti barabara mshambuliaji wa Azam, Prince Dube na kushindwa kufika kwenye lango la Simba akiwa na mpira.

31' Dube anapiga off target akiwa yeye na Manula.

33' Azam wanapiga pasi za mipenyezo, Manula ana-slide na kuokoa jahazi.

34' ⚽ Prince Dubeeeeee, bao safi na maridadi kutoka pembeni, Manula anashindwa kufikia na kuzama nyavuni.

39' Kipree, anajaribu mpira unatoka nje ya lango.

42' Dube anapiga kichwa na mpira unapaa juu ya lango la Simba.

44' Azam wanapoteza mpira, Kyombo anaunasa lakini anapiga fyongo.

45+1' Half time.

55' Almanusura Azam waongeze bao la pili kupitia kwa James Atamingo, save maridadi ya Manula inabakisha ubao ulivyokuwa.

59' 🔁 Zayd na Idd Selemani wanaingia kwa Azam.

62' Yahya Zayd, inagonga besela

63' 🟡 Daniel Amoah anapewa kadi ya njano, simba walifanya counter.

65' Azam na Yanga wanatembeza boli zamu kwa zamu.

65' 🔁 Bocco anaingia kuchua nafasi ya Habib Kyombo.

73' 🔁 Banda na Kibu wanaingia.

79' Muhammed Hussein anajaribu kutokea mbali.

80' 🔁 Kola anaingia kuchukua nafasi ya mfungaji pekee mpaka sasa, Prince Dube.

89' 🟡Yahya Zayd anapewa kadi ya njano.

89' 🟡 Bocco anapewa kadi ya njano kwa kumuwekea mguu Daniel Amoah.

90+2' Simba wanajaribu mara mbili bila mafanikio.

92+3' Full time, Azam anamtwanga Simba baada ya takriban miaka sita bila ushindi. Yanga anasalia kileleni kwa tofauti ya alama 3. Simba anapoteza mechi yake ya kwanza ligi kuu ya NBC.
 
.
IMG_20221010_154836.jpg
 
Nilichoelewa mashabiki wasimba MNA MDOMO SANA nimeona thread za Jana umkiipondea yanga ila sisi kimya tunasubiri dk 90
Lakini kimoyomoyo unatamani kusema mnyama atanyolewa leo!
ila ukikumbuka mipasi ya chama, mautundu ya magic okrah, mauwezo na phili na makontro ya kyombo unaishia kujitapa eti unasubiri dakika 90? hujaona nyuzi ya uto wakijidai ni azam leo?
 
Lakini kimoyomoyo unatamani kusema mnyama atanyolewa leo!
ila ukikumbuka mipasi ya chama, mautundu ya magic okrah, mauwezo na phili na makontro ya kyombo unaishia kujitapa eti unasubiri dakika 90? hujaona nyuzi ya uto wakijidai ni azam leo?
Hao wote uliowataja hakuna anaeweza kupata number Azam
 
Kikosi hiki hapa
 

Attachments

  • FgFaFeyUAAAShDm.jpg
    FgFaFeyUAAAShDm.jpg
    78 KB · Views: 3
Back
Top Bottom