FT: Azam FC 1-0 Simba SC | NBC League, 28/10/2022

FT: Azam FC 1-0 Simba SC | NBC League, 28/10/2022

Hata mkiungana nyie team zisizo na viwanja tunawaua
 
Ni bandika bandua leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, pale miamba ya soka Afrika mnyama mkali mwituni wekundu wa msimbazi, watakapo karibishwa na matajiri wa Azam FC katika kuwania pointi 3 muhimu ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu!

Mara baada ya mnyama kutoshana nguvu na mtani wake wa jadi Jumapili iliyopita na azam kukung'utwa 2-1 na KMC, leo watapata nafasi ya kujiuliza,
ngoma ni saa 1 kamili jioni hii!

Wanalunyasi karibuni, mwana kulitaka mwana kulipewa.

Nguvu moja.

=======

01' Mpira umeanza Benjamin Mkapa.

08' Ayoub Lyanga anajaribu kutoka nje ya 18 lakini mpira unapaa juu ya lango la Simba.

13' Kyombooooo, anakosa bao baada ya pasi nzuri kutoka kwa Okra.

17' Azam wanafika kwenye lango la Simba, Kona. Simba wanasimama imara na kona haina madhara..

22' Simba wanacheza pasi nyingi kuelekea lango la azam, mikono ya Ahmada inawaokoa Azam.

23' Onyango anamdhibiti barabara mshambuliaji wa Azam, Prince Dube na kushindwa kufika kwenye lango la Simba akiwa na mpira.

31' Dube anapiga off target akiwa yeye na Manula.

33' Azam wanapiga pasi za mipenyezo, Manula ana-slide na kuokoa jahazi.

34' ⚽ Prince Dubeeeeee, bao safi na maridadi kutoka pembeni, Manula anashindwa kufikia na kuzama nyavuni.

39' Kipree, anajaribu mpira unatoka nje ya lango.

42' Dube anapiga kichwa na mpira unapaa juu ya lango la Simba.

44' Azam wanapoteza mpira, Kyombo anaunasa lakini anapiga fyongo.

45+1' Half time.

55' Almanusura Azam waongeze bao la pili kupitia kwa James Atamingo, save maridadi ya Manula inabakisha ubao ulivyokuwa.

59' 🔁 Zayd na Idd Selemani wanaingia kwa Azam.

62' Yahya Zayd, inagonga besela

63' 🟡 Daniel Amoah anapewa kadi ya njano, simba walifanya counter.

65' Azam na Yanga wanatembeza boli zamu kwa zamu.

65' 🔁 Bocco anaingia kuchua nafasi ya Habib Kyombo.

73' 🔁 Banda na Kibu wanaingia.

79' Muhammed Hussein anajaribu kutokea mbali.

80' 🔁 Kola anaingia kuchukua nafasi ya mfungaji pekee mpaka sasa, Prince Dube.

89' 🟡Yahya Zayd anapewa kadi ya njano.

89' 🟡 Bocco anapewa kadi ya njano kwa kumuwekea mguu Daniel Amoah.

90+2' Simba wanajaribu mara mbili bila mafanikio.

92+3' Full time, Azam anamtwanga Simba baada ya takriban miaka sita bila ushindi. Yanga anasalia kileleni kwa tofauti ya alama 3. Simba anapoteza mechi yake ya kwanza ligi kuu ya NBC.
wamechana mkeka wangu sitaki kusikia
 
Wale waliokuwa wanasema Simba atafungwa na Azam kwasababu ei Yanga alipata sare kwa tabu ebu njooni mjishike ujinga
𝑼𝒏𝒂 𝒍𝒂 𝒌𝒖𝒔𝒆𝒎𝒂 𝒔𝒂𝒔𝒂 [emoji847]
 
Jamani wa kimataifa imekuaje na ndugu zao Azam? Kwema humu ndani? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom