FT: Azam Sports Frederation Cup(FA): Azam Fc 0-1 Young Africans Sc | 12/06/2023 Mkwakwani Stadium Tanga

FT: Azam Sports Frederation Cup(FA): Azam Fc 0-1 Young Africans Sc | 12/06/2023 Mkwakwani Stadium Tanga

Salute Wana JF...

Naaaaam habari zenu wapenda soka ni matumaini yangu kua mpo Sawa mnaendelea kulipambania Taifa.

Leo ndo ile siku litapigwa pira kukamiana, pira Fainali Kati ya wanalambalamba Azam Fc na Wataalamu wa kutambaza soka Safi ukanda huu wa Afrika mashariki na Kati Dar Young Africans yaani wananchiiiiiiiiiiiiiiiii.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Yanga kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kwani msimu uliopita walicheza na coastal union ambapo Yanga alibeba Kombe hivo ndiye bingwa mtetezi.

Habari njema Kwa Azam ni straika namba moja wa Yanga, Fistoni Kalala Mayele hatokuepo pamoja na Aziz Ki. Lakini hii sio shida kwani kinda hatari Clement Mzize mwenye Goli 6 atakuepo kupambania nafasi ya kua mfungaji Bora, kwani anahitaji Goli moja tu kusawazisha mzani.

Mechi itakujia live kupitia Azam TV burudani Kwa wote kuanzia mishale ya saa 9:00 alasiri.

Update zote zitakuepo kwenye huu Uzi. Nani kubeba ndoo...

Ni Azam au Yanga? Tusubiri!.

home win ,correct score 1-0
 
8C77C53F-2C5D-46E6-86D1-9E17DA2D5733.jpeg
 
Back
Top Bottom