Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, leo itashuka dimbani kuwania kuongeza nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 itakapovaana na Burkina Faso katika mchezo wake wa pili wa Kundi B utakaopigwa saa 5:00 usiku.
Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Larbi Zaouli, huku Twiga Stars ikiingia uwanjani ikiwa na morali kubwa baada ya kuifunga mabingwa watetezi Afrika Kusini kwa mabao 2-1 katika mechi ya ufunguzi.
Endapo Tanzania itashinda mchezo wa leo, itafikisha alama sita na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali kabla ya mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Ivory Coast.
Je, wataendeleza wimbi la ushindi na kutinga hatua ya robo fainali?