FT: Canada 0-3 Morocco | World Cup 2026 | NRG Stadium | 4 Julai, 2026 | Morocco wanafuzu Robo Fainali

FT: Canada 0-3 Morocco | World Cup 2026 | NRG Stadium | 4 Julai, 2026 | Morocco wanafuzu Robo Fainali

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wenza, Canada, hivyo inasubiri mashindi wa mchezo wa Ufaransa dhidi ya Paraguay.

Ushindi huo unaifanya Morocco kuendelea kuandika historia katika michuano hiyo, ikiwa ni mara ya pili mfululizo kufika hatua za juu za Kombe la Dunia.

Mara ya kwanza ilikuwa katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar, ambapo waliweka rekodi ya kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kufuzu hadi hatua ya nusu fainali.

==================


Canada wenyeji wenza wa Kombe la Dunia watajaribu kuandika historia watakapokutana na Morocco jijini Houston, wakilenga kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yao.

Baada ya kuitawala kwa kiasi kikubwa mechi yao ya hatua ya 32 bora dhidi ya Afrika Kusini, Canada walivuna matunda ya uvumilivu wao kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 92, na hivyo kushinda mchezo wao wa kwanza kabisa wa hatua ya mtoano katika historia ya Kombe la Dunia.

Kwa upande wa Morocco, nao walihitaji drama za dakika za mwisho ili kufuzu hatua ya 16 bora. Walisawazisha bao dakika ya 91 dhidi ya Uholanzi kabla ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2, na hivyo kuendelea na safari yao katika mashindano hayo.

===//====
Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya 8 bora, au robo fainali ya kombe la dunia 2026.

Morocco imeweka rekodi ya kutinga hatua hii kwa mara ya pili mgululizo kwa na kiwa timu pekee iliyofanya hivyo kutoka Afrika.

Ushindi wa Mabao 3- 0 unamuondoa mwenyeji mmoja wa mashindano haya ambaue ni Canada


Viva Afrika, Viva Morocco.
 
Hizi timu za waarabu the likes of Kina Egypt, Morocco, Tunisia , Algeria n.k huwa sina mzuka nao kiivo ..... Nawaona kama sio waafrika !

Game ya Leo Morocco akichanga karata vizuri atapenya
 
Mechi mbovu Sana hii Kipindi cha Kwanza, Kila mchezaji anataka kupewa Kadi... Morocco wameshindwa kabisa kupita, Canada wamejaza watu wengi Kati..
 
Morocco kipindi cha pili waache kupaki basi kama wanataka washinde hii mechi na waache kucheza rafu hizi za kijinga wasije wakalimwa kadi nyekundu kwa maana naona huyu mwamuzi anapenda sana kutoa kadi.
 
Refa
Morocco kipindi cha pili waache kupaki basi kama wanataka washinde hii mechi na waache kucheza rafu hizi za kijinga wasije wakalimwa kadi nyekundu kwa maana naona huyu mwamuzi anapenda sana kutoa kadi.
Refa wa epl huyu anagawa tiketi balaa
 
Hizi timu za waarabu the likes of Kina Egypt, Morocco, Tunisia , Algeria n.k huwa sina mzuka nao kiivo ..... Nawaona kama sio waafrika !

Game ya Leo Morocco akichanga karata vizuri atapenya
Huenda kweli jamaa sio waafrika, maana wanakwenda tu mbele wakati wengine wote wamerudi nyumbani
 
Safi kabisa Morocco ninawakubali sana, hata wakicheza na Tanzania nitawashabikia wao.

Wanajiamini bila kuwa na kiwewe kama zilivyo timu zingine za kiafrika na nilijua kama wakishambulia tu wataweza kushinda kirahisi tu.

Huyo kipa wa Morocco Bono nasikia alizaliwa Canada lakini anaichezea nchi ya wazazi wake.
 
Hawa ni wa Afrika wenzetu watake wasitake tutawalazimisha kuwa waafrika hahaaa kwa sauti ya machawa
 
Back
Top Bottom