FT: Chelsea 0 Vs 3 Manchester City | EPL | 12.04.2026 - Stamford Bridge

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Patashika nguo kuchanika inatarajiwa leo wakati Chelsea FC watakapowakaribisha Manchester City katika dimba la Stamford Bridge, kwenye mchezo wa kusisimua wa English Premier League

Chelsea wataingia uwanjani wakisaka ushindi muhimu ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi, huku Manchester City wakilenga kuendelea na ubora wao na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya ubingwa.

Mashabiki wa soka duniani kote wanasubiri kwa hamu kuona nani ataibuka kidedea katika pambano hili kubwa.

Je, Chelsea watatumia faida ya nyumbani, au City wataendelea kutamba?

UPDATES
51: Goal - Nico O'Reilly
57: Goal - Marc Guèhi
68: Goal - Jèrèmy Doku
 
Mimi ni shabiki wa Chelsea ile ya watu wazima akina John Terry, Frank Lampard, Didier Drogba, John Obi Mikel, Eden Hazard, Peter Cec, nk.

Hii Chelsea ya watoto wa Umiseta ni pasua kichwa tu. Hata haileweki. Utoto na ubishoo tu ndiyo mwingi!
 
Arteta hanaga vipaumbele sijui yukoje.
Ametumia nishati kuuubwa kuhangaika na makombe ya mbuzi...kaishia kutolewa yote...FA cup na carabao

Sasa wachezaji wamechoka...Mechi muhimu wakati muhimu wachezaji wamelegea.
As the result the club ends in consecutive trophyless.
 
Fala sana yaani kazingua.
 
Mimi ni shabiki wa Chelsea ile ya watu wazima akina John Terry, Frank Lampard, Didier Drogba, John Obi Mikel, Eden Hazard, Peter Cec, nk.

Hii Chelsea ya watoto wa Umiseta ni pasua kichwa tu. Hata haileweki. Utoto na ubishoo tu ndiyo mwingi!
Vitoto vinashindana kwenda saloon tu kukarikiti nywele.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Chelsea ya Roman Abramovich na hii takataka ya waigizaji wa Holywood.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…