Portugal Yapambana na Colombia Katika Vita ya Kuongoza Kundi K Kombe la Dunia 2026
Kundi K linaweza kushuhudia matokeo ya kushtua huku moja ya timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa kabla ya mashindano, Portugal, ikihitaji ushindi dhidi ya Colombia katika mchezo utakaochezwa jijini Miami ili kujihakikishia kumaliza kileleni mwa kundi.
Colombia tayari imefuzu hatua ya mtoano kwa mara ya tatu mfululizo katika historia yake ya kushiriki Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Uzbekistan na DR Congo. Sasa lengo lao ni kuhakikisha wanamaliza katika nafasi ya kwanza ya Kundi K.
Kwa upande wa Portugal, nahodha wake Cristiano Ronaldo aliweka rekodi mpya kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao katika fainali sita tofauti za Kombe la Dunia. Ronaldo alifanya hivyo wakati Portugal ilipoichapa Uzbekistan mabao 5-0 katika mchezo wao uliopita.
Rekodi ya Kukutana
Huu utakuwa mchezo wa kwanza kabisa kati ya Portugal na Colombia. Hata hivyo, Portugal haijawahi kupoteza katika mechi zake tatu za hatua ya makundi ya Kombe la Dunia dhidi ya timu kutoka Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL), ikiwa imeshinda michezo miwili na kutoka sare mmoja.
Colombia nawaelewa sana, hawawezi kukubali kufungwa na yule 'mzee wao'😂😂 Luis Diaz usiniangushe, piga nyingi za kutosha hao watu ambao waliwatesa ndugu zetu wa Msumbiji na Angola.