FT: CRDB Bank Federation Cup 23/24 FINAL: Dak. 120 | Azam FC 0-0 Yanga SC | Pnt (5-6): New Amaan Complex 2/6/2024. Yanga abeba ubingwa

FT: CRDB Bank Federation Cup 23/24 FINAL: Dak. 120 | Azam FC 0-0 Yanga SC | Pnt (5-6): New Amaan Complex 2/6/2024. Yanga abeba ubingwa

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Hatimae ile siku tuliyokuwa tukiisubiria imefika, ni bonge la mechi kati ya Azam na Yanga katika fainali ya kombe la shirikisho la CRDB

Mechi hii itachezwa majira ya saa 2:15 usiku pale kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar

Je, nini kitatokea katika mtanange huo wa kukata na shoka?

Kuwa nami hapa kuanzia Mwanzo, Katikati na Mwisho wa mechi hii

#CRDBBankFederationCup #KombeLaShirikisho #KombeLaShirikishoLaCRDBBank #TFF #AzamFC #YangaSC #AzamvsYanga

----------------------------------------------------------
Updates 1920 Hours

Kikosi cha Yanga: Diara, Yao, Lomalisa, Bacca, Job (C), Aucho, Maxi, Mudathir, Mzize, Aziz Ki na Pacome

Subs: Mshery, Mwamnyeto, Kibabage, Mkude, Sureboy, Shekhan, Farid, Guede, Musonda...

Kocha : Gamondi Miguel / Musa Ndao
----------------------------------------------------------
Kikosi cha Azam: Mohamed, Lusajo (C), Msindo, Fuentes, Bangala, Bin Zayd, Adolf, Sopu, Kipre Jr, Feitoto, Syllah

Subs: Foba, Chilambo, Amoah, Manyama, Akaminko, Sidibe, Nado, Chiwalanga, Kichindo

Kocha : Bruno Ferry/Yusuf Dabo

----------------------------------------------------------

2015 Hours Kick off

01" Yanga wameanzisha mpira hapa

06" Timu bado zinashambuliana kwa zamu, na zinajaribu kusomana

Azam 0 Yanga 0


10" Azam wanashambulia hapa kuelekea Yanga lakini Abdul Sopu anakuwa offside hapa

15" Presha ya shambulizi ni kubwa kwa Azam lakini wanajaribu kuzima Shambulio la Pacome Zouzoua (0-0)

18" Azam wanapata faulo ila inazuiwa na ukuta wa mabeki wa Yanga

23" Sopu Anapiga kona kuelekea Yanga, chupuchupu Mzize ajifunge inakuwa kona tena... azam wanaipiga inaokolewa Yanga wanashambulia Mzize anakosa goli hapa..

27" Aziz Ki anapiga shuti pale lakini Kipa wa Azam anautoa nje kwa ustadi..

30" Aziz Ki anadondoshwa na Adolf, Yanga wanapata faulo inapigwa pale Mustafa Mohamed anaitoa nje..Kona inapigwa wanaokoa Azam
AZM 0 YNG 0

35" Bado ngoma ngumu 0-0, Yanga wanamiliki mpira zaidi, Pacome anakosa umakini ananyang'anywa mpira

41" Azam wanashambulia kwenda Yanga, Beki wa Yanga wanakuwa imara wanazuia shambulizi (0-0)

45" Azam wanashambulia kwenda Yanga..Kipre anaangushwa faulo...Job anapewa kadi njano

3 dakika kuelekea halftime

45+2 Feitoto anamchezea faulo Lomalisa...Njano kadi kwa Feitoto

HALFTIME AZAM 0 YANGA 0
----------------------------------------------------------
Updates 2120 Hours
KIPINDI CHA PILI KIMEANZA

45" Azam wanaanzisha mpira hapa kuelekea Yanga

51 " Lomalisa anamjaribu kipa wa Azam, mpira unaenda nje..Kona fupi inapigwa anaukata Aucho lakini unadakwa

54" Kadi ya njano kwa Mudathir akimuangusha Kipre kwa kushirikiana na Aucho

61" Yanga wanapata faulo baada ya pacome kuangushwa na Msindo..Faulo inapigwa inaokolewa

67" Yao anarusha mpira kuelekea Azam, naona Aziz ki hajaelewana na Yao mpira unaenda nje..Goal kick
-Yanga wanarudi tena, wanashambulia...Maxiiii anatoa mpira njee

72" Vijana wa Azam wanaelekea lango la Yanga, Lusajo anapiga krosi kuuubwa inaenda nje..Azam wamekosa utulivu

74" Msindo Pasco anaonyeshwa kadi njano kwa kumdondosha Yao.. Freekick kuelekea Azam.. Inapigwa pale na Ki Aziz anatafuta angle ya goli lakini inashindikana mpira nje

75" Guede anaingia kuchukua nafasi ya Mzize

78" Mustafa kipa wa Azam yupo chini na anaonyeshwa kadi ya njano kwa kupoteza muda huku akizuga kaumia kumbe sio

83" Azam kwa kasi wanashambulia...Msindo wa Azam anapiga shuti na mguu wa kulia linakwenda nje inakuwa goal kick (AZM 0 YNG 0)

88" Akaminko James wa Azam anaingia anamtoa Bin Zayd

Mudathir wa Yanga anatoka, Musonda anaingia

89" Maxi Nzengeli anakosa goli hapa mpira unaenda nje

90" Dakika nne za nyongeza bado ngoma ngumu 0-0

90+2" Mwaikenda anapata kadi njano kwa kumzonga mwamuzi, Azam wanapata nafasi lakini Djigui Anazuia

90+4 MKUDE ndani, Maxi Nje..wakati huo Aziz ki anamsukuma Msindo wa Azam..Freekick

Dakika 90 zimeisha Azam 0 Yanga 0

Twende Dakika 30 za nyongeza hadi tupate mshindi, asipopatikana kwenye hizi 30 Dakika tutakwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya Penalti

----------------------------------------------------------


UPDATES 2220 HOURS

EXTRA TIME

90" AZAM wanaanzisha boli hapa tena

91" Yanga wanapata kona, Guede anapiga kichwa unawahiwa na Mustafa Kipa wa azam

95" Guede Offside wakati huo Sopu yupo chini aliangushwa na Aucho... Sopu anatolewa na machela

Kocha Gamondi anaonyeshwa Yellow card

99" Guede na Mustafa wanazozana hapa, Kadi njano kwa Guede J.

100" Sopu nje, Nado ndani anaingia (azam 0- Yanga 0)

103" Adolf anamsukuma Guede, anaonyeshwa kadi njano vilevile kocha wa makipa wa azam nae kadi njano

105" Dakika moja ya nyongeza kukamilisha 15 za kwanza kwenye 30 za nyongeza

Azam wanapata kona baada ya feitoto kushambulia, Nado anaipiga wanashambulia Diara anaiwahii

105+1 " HALFTIME ya dakika 30 za nyongeza AZAM 0 YANGA 0

----------------------------------------------------------

Updates 2235 Hours

105+. " Kipindi cha pili cha muda wa nyongeza kumalizia 30 kinaanza kwa Yanga kusukuma gozi lile la ng'ombe

107" Yao Kwasi anapiga kona kuelekea Azam , Baca anapiga mpira kwa kichwa ila Mustafa anaudaka na anaanguka chini hapa inaonekana kama kaumia

110" Sidibe na Manyama Edo wanaingia kwa Azam... Msindo na Bangala wanaenda nje

113" Bado dakika 7 mpira uishe, Syla wa azam anawekwa chini, Freekick

116" Yanga haraka haraka wanaonana pale Katikati..Yao anashambulia mpira unatoka unakuwa wa kurushwa

118" Lomalisa wa Yanga nje, Mwamnyeto Ndani bado ngoma ngumu hakuna goli

119" Siddibe anapiga kona kuelekea Yanga, in swing corner ile inaenda nje

120+1" Mpira umeisha AZAM 0-0 YANGA, tunakwenda kwenye changamoto mikwaju ya Penalti

----------------------------------------------------------

UPDATES

2300 HOURS Manahodha wa timu zote wanaitwa kwenda kuamua goli la kupigia penalti na nani aanze

Refa anawapa semina kidogo makipa wote wawili

MIKWAJU 5 YA PENALTI

Wanaanza Yanga

Aziz Ki [emoji777] anakosa

Azam wanafuata

Adolf [emoji3514] Anapata

Yanga 0 Azam 1

Guede [emoji777] anakosa

Yanga wamekosa penalti ya 2

Sidibe wa Azam [emoji3581] anapata

Pacome wa Yanga [emoji736] Anapata

Fuentes wa Azam anapiga penalti ya 3 [emoji777] anakosa

Yao Kwasi wa Yanga [emoji736] anapata

2_2

Syla wa Azam anapiga penalti ya 4 [emoji777] anakosa

Mwamnyeto wa Yanga [emoji736] kapata

2-3


Kipre Jr anaenda kupiga ya 5 mwisho [emoji736] kapata

3_3

Aucho wa Yanga [emoji736] kapata

3_4

Manyama wa Azam [emoji736] kapata

4_4 wamekosa 2 wote

Musonda wa Yanga [emoji736] kapata

4-5

Feitoto wa Azam [emoji736] kapata

5-5

Baca wa Yanga [emoji777] kakosa

Lusajo wa Azam [emoji777] kakosa

5-5

Mkude wa Yanga [emoji736] kapata penalti ya 9

Nado wa Azam [emoji777] kakosa penalti ya 9

AZAM FC 5 - YANGA SC 6

FULL TIME 0-0

After Penalties (AZAM 5 YOUNG AFRICANS 6)


2320 Hours Mpira umeisha

Dar es salaam Young Africans ni mabingwa wa CRDB FEDERATION CUP 2023/2024

2330 Hours' Man of the Match ni Ibrahim Abdullah Bacca wa Yanga anapewa zawadi ya Kitita cha Tsh 1,000,000/=

2335 Hours
Legend wa Yanga na Zanzibar, Abdi Kassim "Babi" anampeleka Mwali (kombe) kwenye jukwaa la medali

wakati huo ballboys wanapiga picha ya ukumbusho

2338 Hours

Warembo waliovaa nguo za kijani wanapeleka medali pale kwenye jukwaa, wanaanza Waamuzi wa mechi ya leo wakiongozwa na Arajiga Ahmed... Wanamaliza wanapiga picha ya ukumbusho pia

2343 Hours

Azam wanapanda jukwaani kuvaa medali za nafasi ya pili

2345 Hours

Yanga mabingwa wanaitwa kuelekea jukwaani kupewa Zawadi ya kombe pamoja na medali wakiongozwa na Msheri

2348 Hours

KARIA ANAMPA WAZIRI WA MICHEZO WA ZANZIBAR na WAZIRI NDUMBARO DAMAS nao wa pamoja wanamkabidhi Mwamnyeto kombe hilohilo

YANGA WANAKABIDHIWA KOMBE KUPITIA BAKARI MWAMNYETO NA WANANYANYUA KWAPA KUSHEREHEKEA USHINDI WAO...[emoji1628][emoji471][emoji322][emoji323][emoji3455]


----------------------------------------------------------


Asanteni kwa kuwa nami kuanzia mwanzo, kati na mwisho wa huu mchezo [emoji120]

Hongereni Yanga kwa ushindi, Azam pia hongereni kwa kuwapa Yanga ushindani..jipangeni msimu ujao!

NB: Sikio halizidi kichwa, MKUBWA NI MKUBWA TU.

GAME OVER!
 
Ndani ya siku hizi mbili Yellow nation tumekuwa na wakati mgumu sana Jana Al Nasr kapigwa na Mda si mrefu Dortmund kapigwa Sasa ni Yanga pekee kwenye Yellow nation duniani aliebaki kuokoa jahazi
 
Back
Top Bottom