FT: CRDB Bank Federation Cup 23/24 FINAL: Dak. 120 | Azam FC 0-0 Yanga SC | Pnt (5-6): New Amaan Complex 2/6/2024. Yanga abeba ubingwa

FT: CRDB Bank Federation Cup 23/24 FINAL: Dak. 120 | Azam FC 0-0 Yanga SC | Pnt (5-6): New Amaan Complex 2/6/2024. Yanga abeba ubingwa

Hatimae ile siku tuliyokuwa tukiisubiria imefika, ni bonge la mechi kati ya Azam na Yanga katika fainali ya kombe la shirikisho la CRDB

Mechi hii itachezwa majira ya saa 2:15 usiku pale kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar

Je, nini kitatokea katika mtanange huo wa kukata na shoka?

Kuwa nami hapa kuanzia Mwanzo, Katikati na Mwisho wa mechi hii

#CRDBBankFederationCup #KombeLaShirikisho #KombeLaShirikishoLaCRDBBank #TFF #AzamFC #YangaSC #AzamvsYanga

----------------------------------------------------------
Updates 1920 Hours

Kikosi cha Yanga: Diara, Yao, Lomalisa, Bacca, Job (C), Aucho, Maxi, Mudathir, Mzize, Aziz Ki na Pacome

Subs: Mshery, Mwamnyeto, Kibabage, Mkude, Sureboy, Shekhan, Farid, Guede, Musonda...

Kocha : Gamondi Miguel / Musa Ndao
----------------------------------------------------------
Kikosi cha Azam: Mohamed, Lusajo (C), Msindo, Fuentes, Bangala, Bin Zayd, Adolf, Sopu, Kipre Jr, Feitoto, Syllah

Subs: Foba, Chilambo, Amoah, Manyama, Akaminko, Sidibe, Nado, Chiwalanga, Kichindo

Kocha : Bruno Ferry/Yusuf Dabo

----------------------------------------------------------

2015 Hours Kick off

01" Yanga wameanzisha mpira hapa

06" Timu bado zinashambuliana kwa zamu, na zinajaribu kusomana

Azam 0 Yanga 0


10" Azam wanashambulia hapa kuelekea Yanga lakini Abdul Sopu anakuwa offside hapa

15" Presha ya shambulizi ni kubwa kwa Azam lakini wanajaribu kuzima Shambulio la Pacome Zouzoua (0-0)

18" Azam wanapata faulo ila inazuiwa na ukuta wa mabeki wa Yanga

23" Sopu Anapiga kona kuelekea Yanga, chupuchupu Mzize ajifunge inakuwa kona tena... azam wanaipiga inaokolewa Yanga wanashambulia Mzize anakosa goli hapa..

27" Aziz Ki anapiga shuti pale lakini Kipa wa Azam anautoa nje kwa ustadi..

30" Aziz Ki anadondoshwa na Adolf, Yanga wanapata faulo inapigwa pale Mustafa Mohamed anaitoa nje..Kona inapigwa wanaokoa Azam
AZM 0 YNG 0

35" Bado ngoma ngumu 0-0, Yanga wanamiliki mpira zaidi, Pacome anakosa umakini ananyang'anywa mpira

41" Azam wanashambulia kwenda Yanga, Beki wa Yanga wanakuwa imara wanazuia shambulizi (0-0)

45" Azam wanashambulia kwenda Yanga..Kipre anaangushwa faulo...Job anapewa kadi njano

3 dakika kuelekea halftime

45+2 Feitoto anamchezea faulo Lomalisa...Njano kadi kwa Feitoto

HALFTIME AZAM 0 YANGA 0
----------------------------------------------------------
Updates 2120 Hours
KIPINDI CHA PILI KIMEANZA

45" Azam wanaanzisha mpira hapa kuelekea Yanga

51 " Lomalisa anamjaribu kipa wa Azam, mpira unaenda nje..Kona fupi inapigwa anaukata Aucho lakini unadakwa

54" Kadi ya njano kwa Mudathir akimuangusha Kipre kwa kushirikiana na Aucho

61" Yanga wanapata faulo baada ya pacome kuangushwa na Msindo..Faulo inapigwa inaokolewa

67" Yao anarusha mpira kuelekea Azam, naona Aziz ki hajaelewana na Yao mpira unaenda nje..Goal kick
Gongo wazi wakipigwa itakuwa poa sana!
 
Back
Top Bottom