FT: Czech Republic 1-1 South Africa | World Cup 2026 | Mercedes-Benz Stadium | Juni 18, 2026 | 1:00 Usiku

FT: Czech Republic 1-1 South Africa | World Cup 2026 | Mercedes-Benz Stadium | Juni 18, 2026 | 1:00 Usiku

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Pamoja na kufunga goli la kuongoza katika dakika ya 59 kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Korea Kusini, Jamhuri ya Cheki (Czech Republic) walipoteza mwelekeo na hatimaye kufungwa 2-1. Matokeo haya yanawaacha wakiwa na hamu kubwa ya kurudi katika hali ya ushindi kwenye mechi hii.

Kwa upande wa Afrika Kusini, mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mexico haukuweza kwenda vibaya zaidi ya hapo; mbali na kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo ambao walionyesha nia ndogo sana ya kushambulia, walipata pigo lingine kwa wachezaji wao wawili kuonyeshwa kadi nyekundu (kutolewa nje ya uwanja).

Historia ya Timu Hizi (Uso kwa Uso)​

Jamhuri ya Cheki na Afrika Kusini zinakutana kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa, huku mchezo wao pekee wa awali uliowakutanisha ukimalizika kwa sare ya 2-2 katika Kombe la Mabara la mwaka 1997 (Confederations Cup).
 
Hao Wazulu wapigwe ! Tungeyashangilia ila yatasema tunachukua ajira zao. 2-0
Sasa nyieee, mnaenda kwenye nchi za wenzenu, Wenyeji wanajua afadhali wamepata wawekezaji kumbe mnaenda kuwa vinyozi😅😅😅 tena wa kuajiriwa, au Car Wash attendants.
Wazulu wapo Sahihi.......
 
Sasa nyieee, mnaenda kwenye nchi za wenzenu, Wenyeji wanajua afadhali wamepata wawekezaji kumbe mnaenda kuwa vinyozi😅😅😅 tena wa kuajiriwa, au Car Wash attendants.
Wazulu wapo Sahihi.......
Afrika nzima inawaona hawako sahihi! Acha wavune walichopanda! Ukipanda ubaguzi unavuna ubaguzi!! Afrika nzima inashangilia CZE!! Hadi muda huu wameshaanza kuvuna!! Wako nyuma kwa goli 1, na bado!
 
Ni kweli kabisa, kwenye kikosi kizima cha Afrika ya kusini hakuna mchezaji ambaye anaweza kupata namba na akatamba vizuri kwenye timu ya Yanga au Simba! Labda asajiliwe KMC!
 
Hao South Afrika nilisema ndio watakuwa wa kwanza kufungasha virago na kurejea nyumbani kwani hawana mpira wa kuchezea kombe la dunia wao ni wa ligi za mchangani huku Afrika.

Na wanacheza rafu za kijinga kabisa inayoweza kupelekea wapewe kadi nyekundu. Bure kabisa.
 
Hawa Bora wafungwe tu wawahi kucheza Ngoma, wenzao wanadai Haki zao wao wanafanya nini world cup.
 
Nawaombea Bafanabafana wafungwe mechi zote, watolewe kwenye hatua ya makundi warudi nyumbani wakaendelee na majukumu mengine 🤓🤠
 
Sasa nyieee, mnaenda kwenye nchi za wenzenu, Wenyeji wanajua afadhali wamepata wawekezaji kumbe mnaenda kuwa vinyozi😅😅😅 tena wa kuajiriwa, au Car Wash attendants.
Wazulu wapo Sahihi.......
Hawako sahihi hakuna sheria zinabariki kuuwa watu na kuchoma mali zao ! Zipo sheria za wakimbizi na wahamiaji either halali au halali jinsi ya kushughulika nao sio kazi ya raia kuwapiga na kuwaua wengine.
 
Back
Top Bottom