Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Ni msimu mwingine wa Ligi ya Mabingwa Africa. Leo hapa nyumbani Tanzania ni sikukuu kwa wapenda kandanda hasa soka la kuvutia, Samba Loketo.
Wawakilishi wa Tanzania, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC leo majira ya saa 1:00 usiku atashuka dimbani huko nchini Guinea, kuchuana na Horoya AC katika dimba la Stade General Lansana Conte.
Simba ambao wamejizolea umaarufu linapokuja suala la mechi za kimataifa, wamekuwa wakifanya vizuri sana watashuka dimbani wakiwa na lengo la kupata matokeo mazuri hasa baada ya vinara wa kundi lao Raja kuibomoa Vipers 5-0 katika mchezo uliopigwa jana usiku.
Simba itawakosa baadhi ya wachezaji kama Jonas Mkude, Augustine Okrah, Saido Ntibazonkiza ambao wamebaki nyumbani Tanzania kutokana na sababu mbalimbali.
Mchezo utakuwa mubashara kupitia ZBC2 katika Kisimbuzi cha AzamTv na Chaneli 229 katika kisimbuzi cha DStv.
Karibuni sana kwa live updates...kila la heri kwa mnyama mkubwa mwituni