FT|| Horoya AC 1-0 Simba SC | CAF Champions League | Stade General Lansana Conte | 11.02.2023

FT|| Horoya AC 1-0 Simba SC | CAF Champions League | Stade General Lansana Conte | 11.02.2023

Nawakumbusha tu
Screenshot_20230211-052805.png

Nyie mnaowasema vipers ni vibonde
 
Nikiwa mpenzi kindakindaki wa Yanga, kwenye match hii nawa support Simba wekundu wa MSIMBAZI. Yanga tuwape support watani zetu
Linapokuja suala la hizi timu zetu kuiwakilisha nchi ningeomba sisi mashabiki tuungane kuzishabikia tuweke kando ukolo na utopolo wetu.
Mimi ni mwananchi kindakindaki naweka kando utopolo naisaport Simba mtani wetu rarua hao holoya kama tunavyokuchakazaga huku.
 
Linapokuja suala la hizi timu zetu kuiwakilisha nchi ningeomba sisi mashabiki tuungane kuzishabikia tuweke kando ukolo na utopolo wetu.
Mimi ni mwananchi kindakindaki naweka kando utopolo naisaport Simba mtani wetu rarua hao holoya kama tunavyokuchakazaga huku.
Kama Taifa stars haiwaunganishi ndio sembuse hivi vilabu? Unamdanganya nani? Unajidanganya nafsi yako.

Huko mitandaoni Haji Mañara na huyu boya msemaji wa Simba ndio wanazidi kutia petrol kwenye moto.

Huko mitandaoni msemaji wa Simba anatumia muda mwingi kuisema Yanga, huku Haji Manara akionekana dhahiri ana kisasi na timu yake ya Simba.

At least Ally Kamwe ni bwana Mdogo lakini is far better kuliko haya matutusa mawili ya Simba Haji Manara na Ahmed Ally.
 
Ni msimu mwingine wa Ligi ya Mabingwa Africa. Leo hapa nyumbani Tanzania ni sikukuu kwa wapenda kandanda hasa soka la kuvutia, Samba Loketo.

Wawakilishi wa Tanzania, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC leo majira ya saa 1:00 usiku atashuka dimbani huko nchini Guinea, kuchuana na Horoya AC katika dimba la Stade General Lansana Conte.

Simba ambao wamejizolea umaarufu linapokuja suala la mechi za kimataifa, wamekuwa wakifanya vizuri sana watashuka dimbani wakiwa na lengo la kupata matokeo mazuri hasa baada ya vinara wa kundi lao Raja kuibomoa Vipers 5-0 katika mchezo uliopigwa jana usiku.

Simba itawakosa baadhi ya wachezaji kama Jonas Mkude, Augustine Okrah, Saido Ntibazonkiza ambao wamebaki nyumbani Tanzania kutokana na sababu mbalimbali.

Mchezo utakuwa mubashara kupitia ZBC2 katika Kisimbuzi cha AzamTv na Chaneli 229 katika kisimbuzi cha DStv.

Karibuni sana kwa live updates...kila la heri kwa mnyama mkubwa mwituni
View attachment 2513148
Mungu ibariki SIMBA yetu ifanye vizuri huko iliko
 
Hii mechi makolo kama hamjapigwa goli 3 au zaidi basi nipo hapa
 
Hii game natamani simba aanze kufungwa goli moja ili afunguke na kushinda za kutosha. Akianza kufunga simba atabweteka kutazamia droo
 
Kila la kheri Simba.
Leo tutawafundisha namna ya kucheza hizi game za CAF kwenye group stage.
Amin msiami Mnyama atamtafuna Horoya AC hapo hapo.👊

Stade du 28 Septembre​

 
Back
Top Bottom