FT: Ligi Kuu Bara | Coastal Union 0-3 Simba SC | Al Janoub Mkwakwani 03/12/2022

FT: Ligi Kuu Bara | Coastal Union 0-3 Simba SC | Al Janoub Mkwakwani 03/12/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya kugombea alama tatu muhimu kwenye mchuano wa Ligi Kuu Tanzania Bara[emoji1241] kuendelea kugombewa leo 03/12/ 2022 ambapo wenyeji Wagosi wa Kaya Coastal Union[emoji191] wanawakabili Wekundu wa Msimbazi Simba SC[emoji881] katika Uwanja wa Al Janoub[emoji2522] Mkwakwani Jijini Tanga.

Mechi hii itakuwa ya ushindani wa kutosha ndani ya dimba ambapo Kocha wa Coastal Union Yusuph Chipo amesema, wataona vitu tofauti uwanjani huku Kocha wa Simba Juma Mgunda akisema, yupo kwa ajili ya kutimiza wajibu wake.

"Tumejiandaa vizuri katika mechi yetu dhidi ya Simba SC, mechi iliyopita tulipoteza, lakini tumejirekebisha na tumebadilika, tupo tayari kupambana kupata matokeo ya ushindi, kwahivyo tunaamini tutaona vitu tofauti uwanjani." Amesema Chipo.

"Maandalizi ya kucheza dhidi ya timu nzuri yenye ushindani ya Coastal yamekamilika, vijana wapo tayari kwa ajili ya kupambana ili kupata matokeo mazuri, nimecheza Coastal na nimefundisha Coastal, kwahivyo mchezo wa leo nipo kwa ajili ya kutimiza wajibu wangu kama Kocha wa Simba SC". Amesema Mgunda.

Unadhani Timu ipi imejipanga vizuri kushinda mchezo huu? Yote ni dakika 90 za Jasho na Damu Kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00[emoji354] Alasiri, Usikose Yatakayojiri..!

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

================

00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Mkwakwani | Coastal 0-0 Simba SC

05' Coastal wamepata faulo lakini mpira unapaa na unatoka nje ya lango la Simba.

09' Free Kick ya Chama kuelekea Coastal Henock anashindwa kufunga bao.
15' Majimengi anashindwa kufunga bao, ilikuwa nafasi nzuri kwa Coastal

19' Vicente abubakar anapiga shutii lakini golikipa Manula anacheza na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

25' Sakho anaweka kambani bao lakini mwamuzi anasema ni Offside.
34' Coastal wanapata Kona, lakini mabeki wa Simba wanaokoa hatari ile

Mashambulizi ni kwa pande zote mbili lakini hakuna bao mpaka sasa.
40' Kanoute na Onyango wanaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kupinga maamuzi ya refa.

45+3' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo hakuna bao.
Phiri anadhibitiwa vema na beki wa Coastal, almanusura afunge bao. Naaam mpira ni mapumziko | Coastal Union 0-0 Simba SC

HT: Coastal Union 0-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza Mkwakwani Stadium huku Simba wakifanya mabadiliko ametoka golikipa Manula na ameingia Beno.

Vicent anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya.

51' Phiri anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi lililoanza kwa Chama.

53' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal

General Moses Phiri anaweka kambani bao la kwanza | Coastal Union 0-1 Simba SC

Kapombe anaangushwa eneo la 18, refa aliamuru mkwaju wa penalty

61' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal
General Moses Phiri anaweka kambani bao la pili kwa mkwaju wa penalty

68' Konfor anapiga shutii kali, lakini golikipa Beno anapangua na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

71' Ametoka Sakho na ameingia Okrah, wakati huo huo ni Water break.

76' Coastal wanafanya mabadiliko ya mchezaji huku wakijaribu kupanga mashambulizi kuona kama wanaweza kusawazisha.

82' Ni Free Kick kuelekea Coastal, anakwenda kupiga Chamaa, lakini mpira unatoka nje.

Inapigwa Kona, lakini golikipa Beno anatokea na kudaka bila wasiwasi

89' [emoji460] Chamaaa Goooooooooooooaaal gooal, Simba SC wanapata bao la tatu kupitia kwa Chama, baada ya piga nikupige ya Phiri na Bocco.

90+5' kuelekea kumalizika kwa mchezo
Kanoute anaonyeshwa Kadi Nyekundu baada ya kupata Kadi ya kwanza ya Njano

Ametoka Bocco na Henock, na wameingia Oattara na Akpan

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Coastal Union

FT: Coastal Union 0-3 Simba SC

.......[emoji2788] Ghazwat....
 
HEAD TO HEAD 2017-2022 Simba SC Vs Coastal Union. Hizi hapa takwimu za mechi kumi kabla ya mchezo wa leo.
20221203_134059.jpg
 
Patashika ya kugombea alama tatu muhimu kwenye mchuano wa Ligi Kuu Tanzania Bara[emoji1241] kuendelea kugombewa leo 03/12/ 2022 ambapo wenyeji Wagosi wa Kaya Coastal Union[emoji191] wanawakabili Wekundu wa Msimbazi Simba SC[emoji881] katika Uwanja wa Al Janoub[emoji2522] Mkwakwani Jijini Tanga.

Mechi hii itakuwa ya ushindani wa kutosha ndani ya dimba ambapo Kocha wa Coastal Union Yusuph Chipo amesema, wataona vitu tofauti uwanjani huku Kocha wa Simba Juma Mgunda akisema, yupo kwa ajili ya kutimiza wajibu wake.

"Tumejiandaa vizuri katika mechi yetu dhidi ya Simba SC, mechi iliyopita tulipoteza, lakini tumejirekebisha na tumebadilika, tupo tayari kupambana kupata matokeo ya ushindi, kwahivyo tunaamini tutaona vitu tofauti uwanjani." Amesema Chipo.

"Maandalizi ya kucheza dhidi ya timu nzuri yenye ushindani ya Coastal yamekamilika, vijana wapo tayari kwa ajili ya kupambana ili kupata matokeo mazuri, nimecheza Coastal na nimefundisha Coastal, kwahivyo mchezo wa leo nipo kwa ajili ya kutimiza wajibu wangu kama Kocha wa Simba SC". Amesema Mgunda.

Unadhani Timu ipi imejipanga vizuri kushinda mchezo huu? Yote ni dakika 90 za Jasho na Damu Kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00[emoji354] Alasiri, Usikose Yatakayojiri..!

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Ninacho wakubali Simba na Costal wao wanakubaliana kama ilivyokuwa kwa Mgunda,so washakubaliana leo Simba amfunge ngapi costal.

Costal na Simba ndugu hao, so hongereni Simba kwa kuchukua point zenu tatu.
 
Kikosi cha Coastal Union kimefika Uwanja wa Mkwakwani tayari kukipiga dhidi ya Simba SC
Screenshot_20221203-150524~2.jpg
 
Kikosi cha Coastal Union kinachoanza dhidi ya Simba SC
Screenshot_20221203-152206~2.jpg
 
Wakuu samahani, najua si mahala pake lakini naomba kuuliza.

Kwenye wimbo wa Songa -enzi za utoto kwenye kibwagizo kale katoto kanaongea maneno gani?
 
Back
Top Bottom