Patashika ya kugombea alama tatu muhimu kwenye mchuano wa Ligi Kuu Tanzania Bara[emoji1241] kuendelea kugombewa leo 03/12/ 2022 ambapo wenyeji Wagosi wa Kaya Coastal Union[emoji191] wanawakabili Wekundu wa Msimbazi Simba SC[emoji881] katika Uwanja wa Al Janoub[emoji2522] Mkwakwani Jijini Tanga.
Mechi hii itakuwa ya ushindani wa kutosha ndani ya dimba ambapo Kocha wa Coastal Union Yusuph Chipo amesema, wataona vitu tofauti uwanjani huku Kocha wa Simba Juma Mgunda akisema, yupo kwa ajili ya kutimiza wajibu wake.
"Tumejiandaa vizuri katika mechi yetu dhidi ya Simba SC, mechi iliyopita tulipoteza, lakini tumejirekebisha na tumebadilika, tupo tayari kupambana kupata matokeo ya ushindi, kwahivyo tunaamini tutaona vitu tofauti uwanjani." Amesema Chipo.
"Maandalizi ya kucheza dhidi ya timu nzuri yenye ushindani ya Coastal yamekamilika, vijana wapo tayari kwa ajili ya kupambana ili kupata matokeo mazuri, nimecheza Coastal na nimefundisha Coastal, kwahivyo mchezo wa leo nipo kwa ajili ya kutimiza wajibu wangu kama Kocha wa Simba SC". Amesema Mgunda.
Unadhani Timu ipi imejipanga vizuri kushinda mchezo huu? Yote ni dakika 90 za Jasho na Damu Kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00[emoji354] Alasiri, Usikose Yatakayojiri..!
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
================
00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Mkwakwani | Coastal 0-0 Simba SC
05' Coastal wamepata faulo lakini mpira unapaa na unatoka nje ya lango la Simba.
09' Free Kick ya Chama kuelekea Coastal Henock anashindwa kufunga bao.
15' Majimengi anashindwa kufunga bao, ilikuwa nafasi nzuri kwa Coastal
19' Vicente abubakar anapiga shutii lakini golikipa Manula anacheza na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao
25' Sakho anaweka kambani bao lakini mwamuzi anasema ni Offside.
34' Coastal wanapata Kona, lakini mabeki wa Simba wanaokoa hatari ile
Mashambulizi ni kwa pande zote mbili lakini hakuna bao mpaka sasa.
40' Kanoute na Onyango wanaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kupinga maamuzi ya refa.
45+3' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo hakuna bao.
Phiri anadhibitiwa vema na beki wa Coastal, almanusura afunge bao. Naaam mpira ni mapumziko | Coastal Union 0-0 Simba SC
HT: Coastal Union 0-0 Simba SC
Kipindi cha pili kimeanza Mkwakwani Stadium huku Simba wakifanya mabadiliko ametoka golikipa Manula na ameingia Beno.
Vicent anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya.
51' Phiri anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi lililoanza kwa Chama.
53' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal
General Moses Phiri anaweka kambani bao la kwanza | Coastal Union 0-1 Simba SC
Kapombe anaangushwa eneo la 18, refa aliamuru mkwaju wa penalty
61' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal
General Moses Phiri anaweka kambani bao la pili kwa mkwaju wa penalty
68' Konfor anapiga shutii kali, lakini golikipa Beno anapangua na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.
71' Ametoka Sakho na ameingia Okrah, wakati huo huo ni Water break.
76' Coastal wanafanya mabadiliko ya mchezaji huku wakijaribu kupanga mashambulizi kuona kama wanaweza kusawazisha.
82' Ni Free Kick kuelekea Coastal, anakwenda kupiga Chamaa, lakini mpira unatoka nje.
Inapigwa Kona, lakini golikipa Beno anatokea na kudaka bila wasiwasi
89' [emoji460] Chamaaa Goooooooooooooaaal gooal, Simba SC wanapata bao la tatu kupitia kwa Chama, baada ya piga nikupige ya Phiri na Bocco.
90+5' kuelekea kumalizika kwa mchezo
Kanoute anaonyeshwa Kadi Nyekundu baada ya kupata Kadi ya kwanza ya Njano
Ametoka Bocco na Henock, na wameingia Oattara na Akpan
Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Coastal Union
FT: Coastal Union 0-3 Simba SC
.......[emoji2788] Ghazwat....