FT: Ligi Kuu Bara | Ruvu Shooting 0-4 Simba SC | Stade de Benjamin Mkapa 19/11/2022

Sawa mkuu, lakini kweli ile mechi ya juzi na Singida uliwatazama vizuri wachezaji wa SBS na kisha pitia mechi zao zilizopita...
Singida ni timu ndogo tena sana uo ukubwa mnaowapa wameupata wap? ni vile tu mlitoa sale nao but bado hata uzoefu wa ligi hawana ni kikundi tu kimenunuliwa baada ya timu kupanda daraja
 
Kama kawaida hii mechi ni fainal
 
Tatizo wana simba wabishi mno kukubari
 
Muhimu mpira uchezwe uwanjani. Binafsi nisingependa kusikia malalamiko na visingizio vya kipuuzi! Sijui tulikamiwa! Sijui kocha wao ni Yanga lia lia, hivyo amewaambia wachezaji wake watukamie!!
Jamaa zetu wamekwisha funga ndoa na malalamiko , huwezi kuwatenganisha
 
Timu zote za NBC League zenye Makocha wa Zamani wa Yanga au wachezaji wa zamani wa Yanga ni Hatarishi sana kwa Simba na Simba hatutakiwi kuchukulia poa. Wanachezesha wachezaji wao jihad kulinda maslahi ya timu yao ya zamani.
Angalia;
NAMUNGO yupo NSJIGWA
SINGIDA BS yupo Pluijm
GEITA yupo Minziro
RUVU yupo Mkwasa
Kagera yuko MECK
AZAM yupo KALI ONGARA
IHEFU yupo MWAMBUSI
Marare Hamsini yupo
Hizi timu zooooote Simba atapoteza au kupata sare au kupata matokeo finyu kwa utamaduni wa soka la Bongo.
Simba hakikisha;
Matola
Amri Said
Ulimboka
Julio &
Dennis Kitambi wote wapate timu LIGI KUU tutaanzia hapo kumkamata Yanga vinginevyo kumsimamisha ni ngumu maaana ligi imekaa ki Chupli Chupli
 
Nakumbuka kipindi kile Matola yupo Lipuli asee Yanga tulikoma, hata kipindi Mgunda bado yupo Coastal nakumbuka kuna kipindi alitufunga na mechi nyingi kati Yanga na Coastal zilikua tough sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…