Vumbi la Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kutimka leo Novemba 19, 2022 ambapo Maafande wa Ruvu Shooting[emoji838] wanakiwasha dhidi ya Mnyama Mkali Mwituni Simba SC[emoji881] kwenye Uwanja wa Stade de Benjamin Mkapa[emoji2522] Dar es salaam.
Hii mechi huenda ikawa ya moto sana na ushindani wa kutosha ndani ya dimba kutokana na timu zote mbili kuwa na Makocha Malegendari wa Vilabu nchini Tanzania, Charles Mkwasa na Juma Mgunda.
Kocha Msaidizi wa Ruvu Shooting amesema haya kuelekea mchezo huo. "Tumetoka Uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo, Simba ni timu kubwa na bora tunawaheshimu lakini tutaingia kwa kushindana ili kupata matokeo chanya". Amesema Kocha Msaidizi wa Ruvu.
Naye Kocha wa Simba SC amesema haya kuelekea mchezo huo. "Maandalizi yanakwenda vizuri tuna mechi muhimu na ngumu na utakuwa mchezo wa ushindani, kuhusu Chama amerudi kundini anaendelea vizuri na kwa mapenzi ya mungu kesho (leo) atakuwa kwenye kikosi". Amesema Kocha wa Simba.
Ruvu Shooting wapo tayari kuzuia malengo ya Simba na wao kupata ushindi au Boli Litatembea na wao Simba kupata ushindi.!? Dakika 90 za jasho na damu kuamua.
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00[emoji354] Usiku. Usikose Ukaadithiwa Yaani.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana[emoji2424]