FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 2-0 Kagera Sugar | Uwanja wa Mkapa | Agosti 20, 2022

FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 2-0 Kagera Sugar | Uwanja wa Mkapa | Agosti 20, 2022

Naaam..Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Agosti 20, 2022 ambapo Wataalamu wa kusakata Kabumbu la viwango vya CAF Simba SC Wekundu wa Msimbazi wanatunishana misuli na Kagera Sugar Wanankurukumbi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mbiringe hii huenda ikawa ya hatari na ya kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizingatia Simba anataka kuendelea na ushindi baada ya kutakata mchezo wa kwanza kwa ushindi murua wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold huku Kagera Sugar wakihitaji ushindi baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza 2-1 dhidi ya Azam FC.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amesema kuwa mchezo wa kesho (leo) utakuwa mchezo nzuri na bora zaidi, na watahakikisha wanafanya kitu ambacho wanasimba wanahitaji, timu inapreform na kupata matokeo ya ushindi.

Naye Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza amesema kuwa, Simba SC ni timu kubwa na wanawapa heshima yao, wao wanakwenda kwenye mchezo wa Kesho (leo) kama Underdog, lakini mwisho wa siku mchezo ni dakika 90 ndo zitaamua matokeo.

Anayecheka mwisho ndo anayefurahi zaidi...Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku. Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
SIMBA 3 Kagera 1
 
Saa 10 tunamkanda utopolo.
Tunamalizia saa 1 usiku tunamkanda kagera sugar.
Tunaongoza Tena ligi
 
Back
Top Bottom