FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar | Uwanja wa Mkapa | Juni 23, 2022

FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar | Uwanja wa Mkapa | Juni 23, 2022

Wakiwa wanacheza soka la kuvuta hisia mujarabu na kuburudisha watazamaji walio wengi, soka ambalo limethibitishwa na Shirikisho la Kabumbu Barani Afrika CAF, Mnyama Mkali Mwituni Simba SC leo Juni 23, 2022 atakuwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Jiji Dar es salaam kucheza na Mtibwa Sugar.

Huenda mchezo ukawa na ushindani mkubwa hasa baada mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Manungu Complex kutoka sare ya bila kufungana.

Beki wa mpira Pascal Wawa raia wa Ivory Coast ambaye anamaliza mkataba wake, anatarajiwa kuagwa rasmi kwa kucheza mchezo wake wa mwisho hii leo huku kukiwa na fursa kwa mashabiki kuagana baada ya kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu.

Je mambo yatakwenda kama mchezo wa kwanza? Yote ni dakika 90 kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku. Usikose Ukaambiwa.

Kulitaka Mwana...Kulipewa Mwana

========

Mpira umeanza kwa kasi huku kila timu ikicheza kwa tahadhar kubwa.

10' Mtibwa Sugar wanapata Kona... Lakini mpira unatoka nje wa kurusha

16' Sakho Goooooooooooooaaal
Pape Sakho anaipatia Simba SC bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Kibu | Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar.

18' Mtibwa Sugar wanafanya shambulizi lakini golikipa Beno anarukaaaa kule na kudaka

20' Kihmbwa anatoa pasi ambayo inakuwa fupi kumfikia mfungaji, ilikuwa nafasi nzuri.

25' Free Kick inapigwa kuelekea Simba, Ndemla anapiga shutii lakini golikipa Beno anadaka bila wasiwasi

27' Kibu yupo chini baada ya kupata rabsha, ameinuka mpira unaendelea

30' Simba wanapiga pasi za hapa na pale, kujaribu kupata upenyo kwa Mtibwa.

35' Jimmy anafanya Kazi nzuri, anatoa nje mpira na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

37' Nao Simba walipata Kona.. Lakini mpira unaokolewa na mabeki wa Mtibwa

Free Kick inapigwa kuelekea Mtibwa, Sakho anapiga shutii lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick

40' Mtibwa wameamka sasa, Simba wanautafuta, ngoja Tuone

44' Kona fupi inaanzwa na Sakho kwake Banda Goooooooooooooaaal gooal

Peter Banda anahesabu bao la pili baada ya golikipa Kado kudaka mpira na kumponyoka akiwa ndani. Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar

45+1' Kado na Mhesa waonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumzonga mwamuzi

Sakho anapangua mabeki wa Mtibwa, lakini anaangushwa, huku Kanoute akionyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya.

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanatoka mbele ya mabao mawili kwa bila dhidi ya Mtibwa.

HT: Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, Je mambo yatabadilika..?!

47' Juma anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Sakho

Almanusura Kibu afunge bao, kama si Kado kwenda kuufuata mpira na kumbabaisha

Offside upande wa Mtibwa, huku Simba wakifanya mabadiliko, ametoka Kibu na ameingia Mhilu

56' Simba SC wanacheza soka safi sana, zinapigwa sambusa

Beno anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari langoni kwake, anapangua Shuti kali sana.. Ilikuwa hatari sana

60' Sakho yupo chini baada ya kupata rabsha, anapatiwa matibabu nje

Kagere anapiga Krosi lakini Banda anapiga nje, Kanda ameingia upande wa Mtibwa Sugar akichukua nafasi ya Nassoro.

74' Deo Kanda anajaribu kutafuta mpenyezo kwa mabeki wa Simba, lakini Kennedy anakaa imara

Ametoka Sakho na ameingia Lwanga upande wa Simba, na ametoka Mhesa na ameingia Chota upande wa Mtibwa Sugar

Mtibwa wapo pungufu baada ya Ndemla kuonyesha Kadi Nyekundu kwa kumchezea madhambi Kanoute

80' Mtibwa wanagonga sasa Nyangi kwake Deo, wajaribu kutafuta nafasi

Kagere na Mhilu wanashindwa kutumia nafasi ya Krosi ya Banda kufunga ilikuwa nafasi murua.

85' Mtibwa wanashindwa kupenya ngome ya Simba, hakuna matumaini hapa, ngoja tuone

Kona zimepigwa 7 kwa Simba na 4 kwa Mtibwa, ni Free Kick sasa kuelekea Simba, inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa.

99+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo

Simba wanacheza, kwake Wawa, anapiga kulee kwake Lwanga, mbele kuleee lakini Ame anaokoa

Naaam mpiraaaa umekwishaaaaaa ambapo Simba wanaibuka kidedea kwa mabao mawili kwa bila.

FT: Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar
Umeandika vzr Sana hongera sijajtizama mpira I'll kwa andiko lako hili nikam Niko uwanjani
 
Angalia kipa alipo then utaamua.
1656007308545.jpg
 
Umeandika vzr Sana hongera sijajtizama mpira I'll kwa andiko lako hili nikam Niko uwanjani
Asante sana kwa pongezi mkuu goroko77 kwa kufuatilia mpira kupitia kwenye hili bandiko.

Haya ndo mambo yetu kwa siku zote yaani..!
 
Makolo mjiulize swali moja walikuwa wapi siku zote hao makolo wawili,Kolobanda na Kolosakho?
 
Hizi mechi za kumwagilia moyo mpaka Chiko Ushindi nae anaonekana sio galasa
 
Back
Top Bottom