FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-0 Geita Gold | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Agosti 17, 2022

FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-0 Geita Gold | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Agosti 17, 2022

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Agosti 17, 2022, ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, anakiwasha na Geita Gold kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90, kwa kila timu kuhitaji ushindi na hasa ukizingatia ndo mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili baada ya kufunguliwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023.

Kocha Zaron Maki wa Simba SC amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo) hakutakuwa mchezo rahisi, ni mechi ngumu dhidi ya timu ngumu, licha ya kupata muda mdogo wa kufanya maandalizi dhidi ya Geita, lakini anaamini atafanya vizuri.

Naye Kocha Msaidizi wa Geita Gold Mathias Wandiba amesema kuwa kwa upande wao wamejiandaa vizuri kwasababu wamepata muda wa kutosha kwa kujua wanacheza mechi ngumu dhidi Simba, kwahivyo wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi.

Nani kuibuka na ushindi wa mabao ya kutosha kwenye mtanange huu wa kwanza kwa timu zote mbili Ligi Kuu Tanzania Bara?

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 12: 15 Usiku.. Usikose Ukapata Simulizi

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Mwanakulitafuta,mwanakulipata🤔
 
Moses phiri asipocheza na leo watakuwa wamezingua sana
 
Manula, Kapombe, Hussein, Henock, Ouattara, Akpan, Kanoute, Sakho, Chama, Dejan, Phiri
 
Matokeo yoyote yatakayetokea, Mimi nitaendelea kuwa mnyama mkali Simba.

Nguvu moja
Huku ni kujiandaa kisaikolojia..!!! Na hasa kama mkifungwa utajifanya , mpira una matokeo matatu.. Sare, Kushinda na kushindwa...!! Sasa sijui kwa nini wanaohisi watafungwa huwa mara zote wanaisemaga statement hiyo mapemaaaa..!!
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Khee!
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] utamfunga mdomo nani tena wakati ushakalia SINDANO??
Jamani wasilazimishe furaha kufungwa na yanga inawauma kama wamepigwa sarmat 2
 
Nitakubali matokeo ya mpira lakini sina lawama na Kocha wala Wachezaji.. hakuna timu ambayo haifungwi, au haishindi, au haitoi sare.
Mshauri boss Kizibo asitoe tena ahadi wananchi watamtoa roho mkifungwa
 
Nitakubali matokeo ya mpira lakini sina lawama na Kocha wala Wachezaji.. hakuna timu ambayo haifungwi, au haishindi, au haitoi sare.
Bado ni kujiandaa kisaikolojia tu. Umesahau kuwa Yanga msimu uliopita wa ligi ya NBC 2021/2022 haikufungwa hata mchezo mmoja..!!?? USIJIZIME DATA..!!
 
Hao watoto wa geita wamefanya usajili wa kitoto sana ...imagine unamuachaje yule kipa wao sasa??wakifa nyingi wastafte mchawi nani?
 
Bado ni kujiandaa kisaikolojia tu. Umesahau kuwa Yanga msimu uliopita wa ligi ya NBC 2021/2022 haikufungwa hata mchezo mmoja..!!?? USIJIZIME DATA..!!
Hayo ya kutofungwa kwa msimu mzima wa Ligi yalishafanywa na Simba SC na Azam FC

Kutofungwa au kushinda ama kutoa sare nimemaanisha kwa michuano yote ambayo Klabu inashiriki..!
 
Back
Top Bottom