FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-0 Mbeya City | Uwanja wa Mkapa | Juni 16, 2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Juni 16 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni, mtaalamu mbobezi wa kusakata Kabumbu lililothibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF Simba SC kutoka viunga vya Msimbazi Jiji Dar es salaam, anashuka kwenye Dimba la Benjamin Mkapa kukipiga na Klabu ya Mbeya City, kutoka Jiji la Mbeya.

Je? Nani yupo tayari kuweza kuibuka na matokeo ya ushindi. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.. Usikose Ukaadithiwa.

Kulitaka Mwana.......Kulipewa Mwana

Kikosi cha Simba SC


Beno
Israel
Hussein
Henock
Wawa
Mzamiru
Kanoute
Kibu
Bwalya
Sakho

Kikosi cha Mbeya City

Mandanda
Kunambi
Mwakinyuke
Maganga
Shemvuni
Andambwile
Ibrahim
Jamal
Nonga
Luzio
Ng'odya

Mwamuzi kwa kati ni Ramadhan Kayoko.
=========================

Naaam mpira umeanza Uwanja wa Benjamin Mkapa..Vita vya dakika 90 za jasho na damu.

00' Simba SC 0-0 Mbeya City

03' Kibu Denis anakosa nafasi nzuri ya kufunga baada golikipa mandanda kuuwahi mpira na kuudaka.

07' free kick kuelekea Mbeya City, Bwalya anapiga, lakini mabeki wa City wanacheza kwa kichwa na kuokoa

10' Hussein anapiga free kick nyingine, lakini mpira unaambaa ambaa pembeni ya uwanja.

15' Bado Milango ni migumu hakuna timu imeona lango, Luzio anapiga shutii la mbali lakini linapaa nje ya lango.

Kibu anapiga Krosi lakini inapotea baada ya kukosa mtu wa kupokea

Krosi ya Hussein Kibu anashindwa kutuliza na kuweka kambani, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga bao

21' Umiliki wa Simba SC mpaka sasa huku City wakiwa wamefanya mashambulizi machache.

Kibu yupo chini baada ya kuangushwa eneo la hatari, refa anakataa

27' Shemvuni anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya

32' Kibu anaweka kambani, lakini refa anasema ni Offside..Bado Milango ni migumu huku Simba wakitalawa dimba

Sakho anaangushwa ndani ya box na golikipa wa City ni Penalty, anakwenda kupiga Sakho

Goooooooooooooaaal gooal Simba SC 1-0 Mbeya City

43' Mbeya City wameamka sasa wanashambulia lango la Simba SC inapigwa kuleeeee Nje.

Golikipa wa City yupo chini baada ya kupata rabsha, ameinuka mpira unaendelea

45+2' kuelekea kuwa mapumziko

Simba wanakosa nafasi nyingine ya kufunga hapa, ilikuwa hatari eneo la City

Mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanatoka mbele kwa bao moja kwa bila dhidi ya Mbeya City

HT: Simba SC 1-0 Mbeya City FC
Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa

50' Simba wanajitahidi kutafuta mpenyezo kwa mabeki wa City, lakini City wanakaa imara

Andambwile anakwenda lakini golikipa Beno anadaka bila wasiwasi

Kibu yeye na lango lakini anapiga njeee, namna gani huyu Kibu Denis

City wanapata Kona inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa.

55' Sakho anakwendaaa Goooooooooooooaaal gooal, Sakho anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi ndefu kutoka kwa Mzamiru

Simba SC 2-0 Mbeya City FC

City wanapata Free Kick inapigwa kulee lakini unambabatiza ukuta na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

60' Simba wanakosa nafasi ya kufunga kupitia kwa Kanoute, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga

Nonga anatoka na anaingia Joseph upande wa City

63' Ametoka Sakho na Kibu na nafasi zao zimechukuliwa na Kagere na Banda.

Free Kick inapigwa kuelekea City inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa na golikipa wa City

71' Almanusura City wapate bao baada ya mpira kugonga mlingoti na kuokolewa na mabeki wa Simba

Banda Goooooooooooooaaal gooal

Peter Banda anahesabu bao la tatu akipokea pasi murua kutoka kwa Mhilu

Ametoka Bwalya na ameingia Lwanga upande wa Simba SC

Beno anacheza kwa uzuri, ilikuwa hatari sana, lakini yupo chini, ameinuka mpira unaendelea.

Joseph anapiga shutii lakini nikapaaa njee ya lango

Kagere anapiga shutii, mpira unambabatiza ukuta wa City anatokea Banda anapiga shutii njeee

Beno kwa mara nyingine anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari kuliweka salama lango lake.

Hussein yupo chini baada ya kupata rabsha, ametoka nje kupata matibabu

Free Kick inapigwa kuelekea Simba, lakini Simba wanakataa

Mpira ni mkali kwa pande zote mbili sasa, haya Mhilu anakosa nafasi nzuri ya kufunga

Beno Nyota wa Mchezo anafanya balaa tena, anaokoa mpira wa kichwa

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo

City wanaliandama lango la Simba SC kujaribu kupata walau bao la machozi.

Shemvuni anarudisha mpira wa golikipa wake, anapiga mbele Simba wanawahi

Luzio anapiga shutii lakini golikipa Beno anautema Wawa anaondosha kwenye hatari.

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Mbeya City

FT: Simba SC 3-0 Mbeya City

..... Ghazwat....
 
Inauma Sana Aisee! Wamevuliwa Ubingwa Wa Ngao Ya Jamii, Ubingwa Wa Ligi Kuu Na Ubingwa Wa ASFC Na Yanga Kisha Katika Mechi Nne Zote Walizocheza Msimu Huu Wameshindwa Kuwafunga Yanga Hata Goli Moja Tu Yaani Moja Tu!! [emoji23]...Doooh!! Huu Unyonge Ni Wa Kiwango Cha SGR Kwa Makolo [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…