FT: Ligi Kuu Tanzania Bara | Polisi Tanzania 1-3 Simba SC | Uwanja wa D'eL Ushirika 27/11/2022

FT: Ligi Kuu Tanzania Bara | Polisi Tanzania 1-3 Simba SC | Uwanja wa D'eL Ushirika 27/11/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kuchezwa leo Novemba 27, 2022 ambapo wenyeji Polisi Tanzania wanakiwasha dhidi ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC kunako Dimba la D'eL Ushirika Moshi.

Mechi ngumu kwa pande zote mbili, Polisi Tanzania wakiwa nafasi mbaya ya 13 kutoka chini mwa msimano wa Ligi Kuu wanatafuta kupanda juu huku Simba wakitaka kufuta muendelezo wa matokeo mabaya kwenye viwanja vya ugenini kwa siku za hivi karibuni.

Kocha wa Polisi Tanzania John Tamba amesema haya. "Vijana wapo tayari kuwakabili Simba, kila timu tunaokabiliana nayo kuna maandalizi yake, kwahivyo maandalizi ya kukabiliana na Simba si maandalizi ya kukabiliana na Ihefu kwahivyo kuna mkakati wetu tumeuweka". Amesema Kocha Tamba.

Naye Kocha wa Simba SC Juma Mgunda amesema haya. "Maandalizi yamekamilika na wachezaji wapo na hali nzuri tunajua mchezo utakuwa mgumu, na Polisi hawapo kwenye nafasi nzuri, tunawaheshimu lakini lengo letu ni kupata ponti tatu." Amesema Mgunda.

Yote ni dakika 90 za Jasho na Damu Kufahamika.. Kumbuka mchezo ni saa 10: 00 Alasiri.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

================

00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Ushirika | Polisi Tanzania 0-0 Simba SC.

05' Mashambulizi yanazidi kuelekea lango la Polisi, huku mashuti mawili kutoka kwa Phiri yakikosa kulenga lango.

13' Vitalis manyanga anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Simba.

18' Kipangwile anafanyia faulo, unakuwa mpira wa kupigwa, Athuman anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango.

25' Bocco na Phiri pamoja na Sakho wanakosa utulivu mbele ya mabeki wa Polisi.

29' Simba wanapata Kona ambayo haikuleta matokeo, Kichwa kutoka kwa Kanoute kinatoka nje.

Sakho anaangushwa eneo la 18 lakini Refa anakataa anasema hapana, mpira unaendelea.

32' [emoji460] Bocco Goooooooooooooaaal gooal John Bocco anaweka kambani bao la kwanza | Polisi 0-1 Simba SC.

37' Gadiel anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya, ni free kick kuelekea Simba, inapigwa kulee lakini wanaokoa

Polisi wanapata Kona ambayo haikuzaa bao, mpira Umiliki ni zamu kwa zamu.

43' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal

Moses Phiri anahesabu bao la pili, akipokea pasi murua kutoka kwa Chama.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko

Amsha amsha ya mashabiki wa Simba SC uwanjani wakiwa wapo mbele ya mabao mawili.

HT: Polisi Tanzania 0-2 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza huku Simba wakipata kona ambayo haikuzaa bao.

49' Chama anaonyeshwa Kadi ya Njano baada ya kukataa maamuzi ya refa kisha kuudunda mpira

[emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal

Moses Phiri anaweka kambani bao la tatu akipokea Krosi ya upendo kutoka kwa Chama.

56' Vitalis anapiga tikitaka lakini golikipa Manula anadaka bila wasiwasi.

Polisi Tanzania wanapata Kona, lakini mpira unaokolewa.. huku wachezaji watu wakiingia kuchukua nafasi za wengine.

70' Kennedy ameingia kuchukua nafasi ya Gadiel

Ally Kipemba anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Sakho.

75' Free Kick kuelekea Polisi, anapiga Chama lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick.

88' Ametoka Bocco na ameingia Kibu

90' [emoji460] Goooooooooooooaaal gooal, Polisi wanapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Zubeir Khamis.

90+3 Kuelekea kumalizika kwa mchezo.. Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba wanaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

FT: Polisi Tanzania 1-3 Simba SC

........ Ghazwat...
 
Kikosi
 
Attachments

  • FikaMmAXkAEsq8W.jpg
    FikaMmAXkAEsq8W.jpg
    80.4 KB · Views: 3
Alivyosema Kocha wa City ni kama alivyosema Kocha wa Polisi Tanzania, kujiandaa kwao si kama kujiandaa kwa timu nyingine..!

Nguvu Moja [emoji881]
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kuchezwa leo Novemba 27, 2022 ambapo wenyeji Polisi Tanzania wanakiwasha dhidi ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC kunako Dimba la D'eL Ushirika Moshi.

Mechi ngumu kwa pande zote mbili, Polisi Tanzania wakiwa nafasi mbaya ya 13 kutoka chini mwa msimano wa Ligi Kuu wanatafuta kupanda juu huku Simba wakitaka kufuta muendelezo wa matokeo mabaya kwenye viwanja vya ugenini kwa siku za hivi karibuni.

Kocha wa Polisi Tanzania John Tamba amesema haya. "Vijana wapo tayari kuwakabili Simba, kila timu tunaokabiliana nayo kuna maandalizi yake, kwahivyo maandalizi ya kukabiliana na Simba si maandalizi ya kukabiliana na Ihefu kwahivyo kuna mkakati wetu tumeuweka". Amesema Kocha Tamba.

Naye Kocha wa Simba SC Juma Mgunda amesema haya. "Maandalizi yamekamilika na wachezaji wapo na hali nzuri tunajua mchezo utakuwa mgumu, na Polisi hawapo kwenye nafasi nzuri, tunawaheshimu lakini lengo letu ni kupata ponti tatu." Amesema Mgunda.

Yote ni dakika 90 za Jasho na Damu Kufahamika.. Kumbuka mchezo ni saa 10: 00 Alasiri.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Mkuu Mayele Ana Goli 10 Sasa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakati wowote mpira utaanza Uwanja Ushirika

00' Naaam mpira umeanza | Polisi Tanzania 0-0 Simba SC
 
Ni msako lango la Simba.. Hawa police wangekuwa makini tayari Kuna watu wangekuwa wameoga goli mbili hapa
 
Back
Top Bottom