FT: Ligi ya NBC: KMC 0 vs 1 Yanga S.C: Uwanja wa Benjamin Mkapa, 22/02/2023

FT: Ligi ya NBC: KMC 0 vs 1 Yanga S.C: Uwanja wa Benjamin Mkapa, 22/02/2023

Ushetani umeanza lini?
Mimi mbona ni kawaida yangu?? Ila ww sio kawaida yako yani hupendezi kabisa kuwa na roho ngumu kwetu sisi watani zako.kwani huoni kama mm ushetani unanipendeza? πŸ˜„ πŸ˜„ πŸ˜„ πŸ˜„ πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
 
Mimi mbona ni kawaida yangu?? Ila ww sio kawaida yako yani hupendezi kabisa kuwa na roho ngumu kwetu sisi watani zako.kwani huoni kama mm ushetani unanipendeza? πŸ˜„ πŸ˜„ πŸ˜„ πŸ˜„ πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
Hata hipendezeiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Screenshot_20230222-212930.jpg
 
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Young Africans jioni ya leo majira ya saa 10.00 watashuka katika dimba la Benjamin Mkapa kumenyana na Kinondoni Municipal Football Club ( KMC ) katika mwendelezo wa ligi kuu ya Nbc

Ikumbukwe kuwa Yanga imepata ushindi katika mechi 9 mfululizo za ligi ya Nbc huku KMC wakipoteza mechi zao mbili zilizopita za ligi.

Yanga itaingia uwanjani kusaka ushindi wa 10 mfululizo kwenye ligi ya Nbc huku ikiwa na hamasa kubwa baada ya jumapili iliyopita kupata ushindi mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Tp Mazembe ya DR Congo, hivyo KMC watakuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha wanawazuia Yanga ambao wako kwenye kiwango Bora zaidi.

Usiwe mbali na Uzi huu kwani utakipata kile kitachojili uwanjani

Timu zote tayari zimeshaingia uwanjani na kinachosubiriwa ni Kipyenga cha mwamuzi Isihaka kuashiria kuanza kwa mpambano huu
.........................................

00" Kipyenga kimepulizwa na Kmc waanza mpira

10" Bado milango ni migumu kwa pande zote huku kila timu ikimsoma mpinzani wake

20" Kmc wameanza kufika langoni mwa Yanga ila Shambulizi halikuzaa matunda

32" Yanga wanapata faulo eneo zuri anapiga Aziz Ki ila shuti lake linadakwa na golikipa wa Kmc

38" Gooooal . Yanga wanapata bao la kwanza kupitia Clement Mzize kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Aziz K.

45" Clement Mzize anapiga shuti Kali linagonga nguzo na kurudi uwanjan. Ilikuwa ni Shambulizi la hatari langoni mwa kmc.

HT. Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika huku Yanga wakiongoza kwa bao 1-0. Tukutane kipindi cha pili

Kipindi cha pili kimeanza

65" Clement Mzize anapoteza nafasi ya kuiandikia Yanga goli la pili

84" Mayeeeeeeeeeeee...... Shuti lake Kali linagonga nguzo na kurudi uwanjani

90" Dak 3 Zimeongezwa hapa na mwamuzi.

Naam mpira umekwisha Yanga wakiondoka na ushindi wa bao Moja Kwa bila na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha alama 62 na kuwaacha wapinzani wake Simba wenye alama zao 54.
Tukutane wakati mwingine. Jioni njema
Najiuliza, kocha ws makipa wa KMC ni nani? Siamini kama ni Juma Kaseja.
Mechi hii kipa alikuwa anawazawadia Yanga bao mbili za uhakika.
 
Back
Top Bottom