FT: Mamelodi Sundowns 2-0 Wydad (Agg: 3-2)AC | African Football League Final | 2nd Leg | Loftus Versfeld Stadium | 12.11.2023. Mamelodi bingwa

FT: Mamelodi Sundowns 2-0 Wydad (Agg: 3-2)AC | African Football League Final | 2nd Leg | Loftus Versfeld Stadium | 12.11.2023. Mamelodi bingwa

OC-CID

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2023
Posts
200
Reaction score
463
Leo kunapigwa mchezo wa Fainali ya African Football League mkondo wa pili.

Ni Mamelodi Sundowns Vs Wydad Athletic Club saa 10:00 jioni katika dimba la Loftus Versfeld jijini Pretoria.

Katika mkondo wa kwanza Wydad alishinda 2-1.

Leo kazi ni moja tu kwa Mamelodi kuibuka na ushindi na kutwaa ndoo ya kwanza ya mashindano hayo mapya barani Afrika.

#######

MAMELODI BINGWA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE 2023
Timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imebeba ubingwa wa The African Football League 2023 kwa kuitandika Wydad Casablanca ya Morroco magoli 2-0 katika Fainali ya Pili.

Kutokana na matokeo hayo, Mamelodi imeshinda kwa jumla ya magoli 3-2 kwa kuwa katika Fainali ya Kwanza Wydad AC ilishinda magoli 2-1.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria umekamilisha safari ya Michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza ilishirikisha timu nane ikiwemo Simba ya Tanzania.
 
Leo kunapigwa mchezo wa Fainali ya African Football League mkondo wa pili.

Ni Mamelodi Sundowns Vs Wydad Athletic Club saa 10:00 jioni katika dimba la Loftus Versfeld jijini Pretoria.

Katika mkondo wa kwanza Wydad alishinda 2-1.

Leo kazi ni moja tu kwa Mamelodi kuibuka na ushindi na kutwaa ndoo ya kwanza ya mashindano hayo mapya barani Afrika.
All the best Masandawana
 
Yanga katika safari yetu ya kufika fainali ya caf champions league msimu huu.

Tunapiga wote walioshiriki bonanza la kusema washiriki wote wanaanzia robo.

Ujinga mtupu ni Mashindano gani yanaanziaga robo fainali?
Aaahaaa

Eti tunawapiga wote walioshiriki bonanza
 
Nataka Mamelody ashinde ila class ya wydad kwa Sasa iko juu Yao so naiona Wydad ikishinda hii game japo Jaburane hayupo Leo
Team pekee ya kumfunga Wydad kwa Sasa ni Yanga
😄😄😄😄
 
Yanga katika safari yetu ya kufika fainali ya caf champions league msimu huu.

Tunapiga wote walioshiriki bonanza la kusema washiriki wote wanaanzia robo.

Ujinga mtupu ni Mashindano gani yanaanziaga robo fainali?
Wataanzaje na mtoano wakati mautopolo yote hayamo kwenye AFL? Wanaazia stage za kibingwa kwa sababu washiriki wote wanastahili kuwa bingwa.
 
Back
Top Bottom