FT: NBC Premier League | Young Africans 5-0 JKT Tanzania | Azam Complex Stadium, Chamazi | 29/08/2023

FT: NBC Premier League | Young Africans 5-0 JKT Tanzania | Azam Complex Stadium, Chamazi | 29/08/2023

Wakipekee

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
6,194
Reaction score
10,711
Habari wanamichezo wa JF? Bila Shaka mpo poa mkiendelea na majukumu yenu ya kulijenga Taifa.

Leo bingwa mtetezi wa ligi namba tano Kwa Ubora barani Afrika namaanisha NBC PREMIER LEAGUE, Dar Young Africans maarufu kama Yanga SC watakua wenyeji wa JKT Tanzania. Mchezo utakaanza mishale ya saa moja kamili kutoka viunga vya Chamazi complex stadium pale mbagala.

Hii itakua mechi ya pili Kwa Yanga ambayo mechi yake ya Kwanza ilimkandamiza bila huruma KMC FC Bao tano Kwa nunge. Pamoja na hayo lakini Yanga ilipiga pasi nyingi kiasi cha kufanya watazamaji wabaki Meno nje Kwa furaha ya soka Safi la pasi nyingi maarufu kama Pira Gamondi.

Kwa upande wa JKT Tanzania wao mechi ya Kwanza walipata ushindi muhimu mbele ya wauaji wa kusini Namungo FC Kwa kusinda Goli 1 bila. Bao lilipachikwa na kiungo wao fundi Martin Kigi na kujihakikishia pointi tatu muhimu.

Katika mechi tano za mwisho Kati Yao, Yanga kashinda mechi nne huku JKT Tanzania wakiambulia Sare moja Tu ya Bao moja Kwa moja. Mechi ya mwisho kukutana Yanga walishinda Bao mbili bila, Goli zikifungwa na mawinga Kisinda na na Yakuba songne. Je, Yanga wataendeleza utabe wao au JKT Tanzania watafuta uteja?

Kwa hayo na mengine mengi, Basi andaa macho na masikio leo saa 1:00 jioni katika dimba la Azam Complex Stadium Chamazi Moto Utawaka. Updates zote utazipata kupitia huu Uzi..

Kila la kheri Wananchi [emoji169][emoji172]
#Daimambelenyumamwiko
 
Back
Top Bottom