FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Mechi inapogwa muda huu, mpaka sasa ni kipindi cha mapumziko Niger 0 Tanzania 0
==

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeanza vizuri Kuwania Kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Niger goli 1-0, mfungaji akiwa ni Charles M’mombwa katika mchezo wa Kundi E.

Mtanange huo umepigwa kwenye Uwanja wa Marrakech Nchini Morocco huku Niger ikitambulika kuwa nyumbani baada ya viwanja vyao kutokidhi vigezo vya ubora unaohitajika.

Mchezo unaofuata kwa Tanzania ni dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Mkapa mnamo Novemba 21, 2023. Timu nyingine katika kundi hilo ni Zambia na Congo wakati Eritrea ilijitoa kwenye ushiriki.

1700326912796.png

F_O5_6iXwAER2gh.jpeg

F_O5_6hWUAAtP7s.jpeg

F_O5_6jX0AA5x1Q.jpeg
 
Kuna huyu beki wa kati kati sijui anaitwa nani yaani garasa tupu bute kabisaa kampasia mpira adui ndani ya box pia anachojua yeye ni kirudisha mpira kwa kipa kidogo achomeshe mara nne
 
Mudathir na kibu sijawaona, alafu hawa wachezaji wa nje nao ni bure kabisa hamna kitu, wanazidiwa na Feitoto
 
Namba 9 pia anapwaya sijui kwanini mzize hajaitwa
 
Dakika ya 49' Taifa stars tunacheza ujjnga
 
Back
Top Bottom