Kingfish23
JF-Expert Member
- Aug 22, 2022
- 490
- 485
Watu mnasahau kwamba Morocco tuliwashona 3 Kwa Mkapa wenyewe wanatuogopaTukiongeza mazoezi ya pumzi na kukaba tukashikilia bomba hatufungwi na Morocco, ila tukifunguka tutapigwa nyingi. Lazima tuwaheshimu, faulo nje ya box hazitakiwi kabisa. Hawa mpira wao kama waarabu wengine hawana jipya na hawajui tunachezaje itatubeba!
Feisal bado sio yule, hivi sasa ni mzito sana muda wote anawaza kurudisha mipira nyuma sijui mbele anaogopa nini , mechi ya Morocco inamhitaji Mudathir tu katikati.
Samatta aache utozi, goli alilokosa akiwa yeye na kipa ni la kijinga kabisa, ila bado ni tegemeo letu mpira anaujua na amebadilika hivi sasa anakaba sana na kusaidia sana timu kule mbele. Kipa wa Niger alisumbuliwa sana na Samatta big up!
Ushindi dhidi ya Morocco pia upo tukitulia mwarabu anakaa tu kwa Mkapa hatoki Mtu, namuona Msuva akipiga goli mbili safi. Point 3 za Morocco tuzipambanie zitatubeba sana. Hii timu iko vizuri sana kushikilia bomba lazima tuseme ukweli
Sent from my TECNO BF7 using JamiiForums mobile app