FT: Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC | Ligi ya NBC | Aprili 8, 2026 | CCM Kirumba

FT: Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC | Ligi ya NBC | Aprili 8, 2026 | CCM Kirumba

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Leo Aprili 8, 2026, mashabiki wa soka nchini wanatarajia kushuhudia pambano kubwa la kusisimua kati ya Pamba Jiji FC na Yanga SC katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC. Mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, kuanzia saa 10:15 jioni.

1775630931807.png
Pamba Jiji FC, wakiwa nyumbani, wataingia uwanjani wakiwa na hamasa kubwa ya kutumia faida ya mashabiki wao kujihakikishia matokeo chanya. Kikosi hicho kimekuwa kikionyesha ushindani mzuri katika mechi za hivi karibuni, na watakuwa na kibarua kizito mbele ya mabingwa watetezi.

Wana Tipilindanda, wamecheza mechi 9 dimba la nyumbani, wakishinda 5, Sare 4 na hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.

Kwa upande wa Yanga SC, wanakuja kwenye mchezo huu wakiwa na morali ya juu wakilenga kuendeleza ubabe wao katika ligi. Wamecheza Mechi 9 Ugenini, Wakishinda 8, Sare 1 na hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.
 
Max kiwango kimeisha mechi nyingi msimu huu performance yake ni ya kiwango cha chini mno
 
Mvua inqnyesha Arusha, alaaaa kumbe mechi aichezwi huku hahahahahahahahah
 
Max kiwango kimeisha mechi nyingi msimu huu performance yake ni ya kiwango cha chini mno
Na sijui kwanini hapumzishwi mwili angalau upate ufanisi tena. Anaonekana tu lakini kocha anamkazania kucheza.
 
Back
Top Bottom