FT: Pre-season International Friendly Match | Simba SC 6-0 Al Akhood Club

FT: Pre-season International Friendly Match | Simba SC 6-0 Al Akhood Club

Wiki moja, game moja, utopolo wasije na ule utopolo wao wa Simba SC imefungwa 12-0!
Walivyo wajinga siku ya game kuna picha ya nyota wa goli bora la CAF Sakho ilhali yeye alikuwa Rabat nchini Morocco.

Yaani hata editing yao inakwenda kiutopolo topolo tu yaani.
 
Klabu ya Simba imejitupa uwanjani hii leo kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki (International Friendly match) dhidi ya Al Akhaood Club, ambapo matokeo ni kuwa Simba SC imeibuka na ushindi mnono wa mabao sita kwa bila.

Huu ni mchezo wa pili kwa Simba baada ya kutanguliwa na ule wa Ismailia SC ambao matokeo yalikuwa ni kutoshana nguvu kwa sare ya bao moja kwa moja, ambapo bao la Simba likifungwa na Nyota Augustine Okrah.

Kwenye mchezo wa leo Julai 23, 2022 matokeo ni haya | FT: Simba SC 6-0 Al Akhaood Club.

Wafungaji Simba SC.

Moses Phiri
Jonas Mkude
Maddie kagere
Pape Sakho
Pape Sakho
Erasto Nyoni

View attachment 2301631
Hii nimekumbuka ishu moja wakati niko O-level kuna jamaa walikuwa wanaishi gheto kwa ajili ya kupiga msuli, baadae wakawekeana utaratibu wakutungiana mitihani.

Wakawa wanapiga A+ kila mitihani Aaah dharau zikahamia darasani kuwa wao wakali hahahah si ikaja mitihan ya muhula kila mtihani unaotoka D na mingine wanazingua kabisa mpaka F.

Ndo nilipojua kuwa kipimo cha ubora ni kwenye uwanja wa mashindano na sio uwanja wa mazoezi.
 
Mmechukua Mashabiki 11 Waliokuja Kuangalia Mazoezi Yenu Mmechz Nao Mechi Af Mnasema Mmechez Na Timu Ya Saudi Arabia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari zetu wao wanazo ila habari zao sisi hatuna. Ama kweli Simba SC ni Taifa Kubwa.
habari zao zipo

20220724_092932.jpg
 
Back
Top Bottom