FT: Senegal 5-0 Iraq | World Cup 2026 | BMO Field | 26 Juni, 2026 | 4:00 Usiku

FT: Senegal 5-0 Iraq | World Cup 2026 | BMO Field | 26 Juni, 2026 | 4:00 Usiku

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205

Senegal na Iraq Zatafuta Ushindi wa Kwanza Kombe la Dunia 2026​

Senegal na Iraq zitashuka dimbani zikiwa na lengo la kumaliza hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa ushindi, katika mchezo wa Kundi I utakaopigwa mjini Toronto. Timu zote mbili bado hazijapata ushindi kwenye mashindano haya, na ushindi unaweza kuzifanya zibakize matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora kama moja ya timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu.

Senegal walikuwa na matarajio makubwa katika Kombe hili la Dunia, ambalo ni la tatu mfululizo kwao. Hata hivyo, mambo hayajawa mazuri hadi sasa baada ya kupoteza michezo yao miwili ya kwanza, wakifungwa Ufaransa mabao 3-1 na Norway mabao 3-2.

Ka upande wa Iraq, hili ni Kombe la Dunia la pili pekee katika historia yao. Kufuzu kwao kulikuwa mafanikio makubwa, lakini walijua wangekutana na ushindani mkali kutokana na kundi walilopangwa.

Rekodi ya Kukutana​

Senegal na Iraq hawajawahi kukutana katika historia. Hata hivyo, Senegal hawajapoteza katika mechi zao mbili za awali dhidi ya timu kutoka bara la Asia kwenye Kombe la Dunia, wakishinda mmoja na kutoka sare mmoja.

Screenshot 2026-06-26 184814.png
 
Senegal walienda wakiwa wamelewa sifa ya kutwaa taji la Afcon lakini ukweli ni kwamba ubora wao ulikua hautoshi na ndio maana wameumbuka haraka sana.

Senegal hawana beki japo kipa wao Edward Mendy anajitahidi sana na wasipoangalia wanaweza kuvuta mkia kwenye kundi lao.
 
Aliyeweka matokeo hapo juu aamke kutoka usingizini halafu aweke matokeo halisi ya 5-0. Na siyo 3-0.
 
Jamaa washavuka, sijui watakutana na England au vipi?....Mechi za Ivory Coast Vs Norway na Morocco Vs Netherlands...hizi mechi lazima timu moja au zote za Afrika itavuka.
 
Back
Top Bottom