Hello Tanzania, Sawubona South Africa!
Karibuni katika Kindumbwe ndumbwe cha mtanange wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Africa (Total Energies CAF CC) kati ya wenyeji Simba Sc wa Tanzania na Orlando Pirates wa South Afrika unaochezwa katika dimba la uwanja wa Taifa, "Kwa Mkapa" leo tarehe 17.04.2022 saa 1 jioni kwa saa za Africa Mashariki (saa 12 jioni kule kwa Madiba Bondeni)
Ni mchezo muhimu kwa timu zote 2 hasa ukizingatia hatua hii ni ya mtoano na mechi ni 2 tu nyumbani na Ugenini, kuelekea nusu fainali. Wenyeji Simba wamefuzu hatua hii ya robo fainali baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi lao D kwa Point 10 nyuma ya RS Berkane ambao nao walikuwa na point 10 pia ila waliwazidi Simba idadi ya magoli ya kufunga. Kwa upande wao Orlando Pirates wao walifuzu hatua hii ya mtoano baada ya kuibuka kidedea katika kundi lao B kwa kuondoka na point 13.
Ni mchezo unaotarajiwa kuwa wa kasi, nguvu, maarifa na akili nyingi kwani Simba wanahitaji kujihakikishia ushindi nyumbani kwa kutaka magoli mengi ili njia iwe nyepesi wanapoenda ugenini huku Orlando Pirates nao wakitaka kulinda heshima kwa Sare au ushindi ugenini ili wapate mtaji mzuri wa kuanzia wakiwa uwanja wao wa Nyumbani "Orlando Stadium". Ikumbukwe hii ni mechi yao ya kwanza kukutana, huko nyuma hawajawahi kuchuana katika mashindano yoyote.
Orlando Pirates yuko nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi yao huku Simba akiwa nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi kuu bara
Je, nani ataibuka kidedea? au itakuwa Suluhu/Sare?
Karibu na kaa nami kuanzia mwanzo, katikati na mwisho wa kipute hiki...
Vikosi huenda vikawa (Sio rasmi)
Simba vs Orlando Pirates Predicted XI
Simba (3-4-3): Aishi Manula (GK); Mohamed Husseini, Joash Onyango, Henock Baka; Bernard Morrison, Jonas Mkude, Peter Banda, Shomari Kapombe; Larry Bwalya, Pape Sakho, Chris Mugalu
KOCHA: Pablo Franc Martin
Orlando Pirates (4-3-3): Richard Ofori (GK); Bandile Shandu, Thulani Hlatshwayo, Happy Jele, Bongani Sam; Abel Mabaso, Goodman Mosele, Kabelo Dlamini; Fortune Makaringe, Deon Kavendji, Kwame Peprah
KOCHA: Mandla Ncikazi
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Updates
1100 HRS
Mechi itaoneshwa kupitia
(ZBC 2 Channel namba 406)- AZAM TV
(Channel 225 FOOTBALL- DSTV )
TV3 (Startimes- channel #197 Dish na #131 antenna)
Streaming Link
www.hesgoal.tv
Sent from my M2101K6G using
JamiiForums mobile app
View attachment 2190564