FT: Simba 1 - 1 Asec Mimosas | CAF Champions league | Mkapa Stadium | 25.11.2023

Changamoto katika timu ni suala la kawaida wewe shabiki wa juzijuzi. Timu haiwezi kuwa kwenye peak muda wote. Kuweni wavumilivu, timu itainuka tena. Manchester, Liverpool, Chelsea zote zimepitia changamoto, lakini mashabiki wamebaki na timu zao.
Wewe ndiye unajua maana ya ushabiki, alafu Simba haijaporomoka kwa kiwango kikubwa kama tunavyoimbiwa humu.
 
Simba bado ni mbovu. Kwa bahati mbaya Viongozi wa Simba na Wachezaji hawalioni hili kabisa. Bado ni mbovu kila kona.

Wakati mwingine pia ifike mahali tusiabudu Wazungu kupita kiasi...yaani Kocha lazima awe mzungu? Kama hamtaki makocha wa kibongo..nendeni mkalete Wasenegal, Wanaigeria, Waivorycost...yaani zipo nchi Afrika zina makocha wazuri tu na wengine walicheza ligi za Uingereza, Ufaransa, Ujerumani n.k

Jambo jingine..baadhi ya viongozi haswa Wazee wasiwe last sayers na kocha pia asiwe last sayer...washirikiane...ndo maana kuna benchi la ufundi.

Simba bado mbovu.
 

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…