FT: Simba S.C 6 Majimaji 1.... Ibrahim Ajibu is back

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Ibrahimu Ajibu "Mzee wa Ma Hat-Trick" is baack.. ndivyo waweza kusema.. na hii ni baada ya kuonesha man of the match performance katika mechi dhidi ya Majimaji ambapo Mnyama kashinda goli 6-1.

Magoli ya Mnyama yamefungwa na Ajibu 8, 11, 42, Kiiza 37, 83 na Mohammed Husein 79.

Achana na ile rekodi ya Ibrahim Ajibu katika msimu uliopita.. ya kutupia goli 3 za haraka zaidi tangu ligi ianzishwe miaka kibao iliyopita.. alitumia Dk. 21 tu kuingia katika rekodi.

Leo tena kaweka rekodi nyingine pia kwa kutupia goli mbili za haraka zaidi tangu ligi ianzishwe miaka kibao iliyopita.. Dk. 3 tu [Dk. 8 na Dk. 11]... zilimtosha kuingia tena katika vitabu vya rekodi ya soka letu nchini.. na ilibakia kidogo tu aivunje rekodi yake ya msimu uliopita.

Wapinzani wetu mjipange kisawa sawa zaidi.. Maana Ibracadabra is baaaaaaaaack.

Nikiripoti toka Taifa Stadium, ni Mimi sembo wa Simba TV.
 
Safi sana mnyama kwa kuwa watafuna maji maji
 
Hongera SSC. Simba tangu iifunge Yanga 5-0 mwaka jz haijawahi kushinda zaidi ya goli 5.
 
Japokuwa imepata ushindi mnono PAKA LA MSIMBAZI Bado halijaweza kutinga katika zile nafasi za Wanaume Yaani Tatu BORA katika msimamo wa ligi.
 
Japokuwa imepata ushindi mnono PAKA LA MSIMBAZI Bado halijaweza kutinga katika zile nafasi za Wanaume Yaani Tatu BORA katika msimamo wa ligi.

Tunakimbiza mwizi kimya kimya.. Hutaamini nafasi tutakayokua ligi itakaposimama kwa ajili ya mapumziko.
 
Tunakimbiza mwizi kimya kimya.. Hutaamini nafasi tutakayokua ligi itakaposimama kwa ajili ya mapumziko.

Hahaha dalil ya mvua ni mawingu. Kila la heri na ndoto zenu. Sisi na shost yenu azam tunabadilishana tuu TOP SEAT kwa raha zetu
 
Mkishakutana na mteremko basi mataaaaambo,.majimaji walikuwa wanashangaa uwanja si unajua toka ujengwe hawajawahi kutia mguu:what:
 
Toto, Azam list inaendelea. Bado sana kujitamba mkuu safari mbele yenu bado kubwa. Jitahidini sana somehow kikosi chenu sasahivi kipo vizuri.

Nashukuru kwa kukiri kua kwa sasa hivi tupo vizuri.. Ila nikupe taarifa tu.. Simba hii bado sana.. Nadhani round ya 2 tutakua katika ubora wetu.
Moderator #BringBackVitufeVyaLike..
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…